Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma DAVID MISIME - SACP
Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
linawashikilia watu nane (8) wanaojihusisha na uhalifu wa makosa mbalimbali ya
uhalifu yakiwepo ya kumiliki silaha kinyume cha sheria, kupatikana na bangi pamoja
na pombe ya moshi katika masako uliofanyika tarehe 04/03/2014.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema katika Wilaya ya
Kongwa amekamatwa mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la MALUGUSO S/O MUNZE,
Mgogo, Mkulima wa MBANDE akimiliki silaha aina ya gobole bila kibali na ni
kinyume na sheria ya kumiliki silaha hiyo.
Pia Kamanda MISIME amesema katika Wilaya
hiyohiyo amekamatwa mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la NGELISHOM S/O LEGUMA
mwenye miaka 40, Mkaguru, Mkazi wa Vihingo Wilayani Kongwa kwa kosa la kukutwa
na kete kumi (10) za Bhangi pamoja na NGEMAUYU D/O JUMA mwenye miaka 34, Mgogo
pamoja na NENELWA D/O OLOTI mwenye miaka 30 wote wakazi wa Ngomai Tarafa ya
Mlali akiwa na Pombe haramu ya Gongo Wilayani Kongwa.
No comments:
Post a Comment