NDLOVU (KULIA) AKIWA NA MALASHI |
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) tumepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) kukamata sh. milioni
106 za klabu ya Yanga kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi zake ili
kuwalipa waliokuwa wachezaji wake Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.
Ukiwa na Habari au matukio tutumie kupitia namba yetu ya
Whatssap 0713966552 au email address sekdavid64@hotmail.com
Tayari tumeanza utekelezaji wa amri
hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Rhino Rangers
iliyochezwa Machi 22 mwaka huu mjini Tabora tumezuia sh. 9,221,250 ambazo ndizo
zilizokuwa mgawo wa Yanga katika mchezo huo ulioingiza jumla ya sh. 38,655,000.
Wachezaji hao walifungua kesi kortini
kupinga mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa haki zao za kimkataba.
Malashi na Ndlovu walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo ya sh.
milioni 106.
Tunawakumbusha wanachama wetu (klabu
za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na vyama shiriki) kuzingatia
mikataba wanayoingia na watendaji wao wakiwemo wachezaji, makocha na maofisa
wengine.
Iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment