Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti
wa CCM Iringa Vijijini Mama Delfina Mtavilalu mara baada ya kuwasili
katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa ambapo alipokelewa na baadhi ya
viongozi wa mkoa huo na kuelekea moja kwa moja ofisini ambapo alifanya
mazungumzo mafupi na viongozi hao na baadae akakutana na waandishi wa
habari, Akizungumza na waandishi wa habari amesema yeye hakkwenda iringa
kupiga kampeni kwakuwa kampeni zinapigwa na kamati za siasa pamoja na
viongozi mbalimbali kutokana na jinzi walivyopangiwa kazi yake yeye ni
kuratibu kampeni hizo na kupokea taarifa za kampeni hizo na kuona kama
kamati za siasa za kata zinafanya kazi, Chama cha Mapinduzi kiko katika
kampeni jimbo la Kalenga pamoja na vyama vingine kikiwa kimemsimamisha
Bw. Godfrey Mgimwa ambapo uchaguzi wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika
Machi 16 mwaka huu.Akizungumza
na waandishi wa habari huku akionyesha moja ya gazeti lililowahi
kuripoti kampeni hizo kwa picha Philip Mangula amelaani kampeni alizodai
zinadhalilisha watoto zinazofanywa na CHADEMA huku akionyesha mmoja wa
watoto ambaye alipigwa picha huku akionyesha sare zake za shule ambazo
zimechakaa na kuchanika na mmoja wa wapiga debe wa chama hicho akisema
kutangaza umasikini wa mtu ni kumdhalilisha Philip
Mangula akiingia katika ofisi za mkoa wa Iringa huku akiwa ameongozana
na Katibu wa Mkoa wa Iringa Bw. Hassan Mtenga na viongozi wengine. Kipande Cha Gazeti hilo kikionyesha picha iliyochapishwa hivi karibuni inayodaiwa kumdhalilisha mtoto. Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akielezea zaidi kuhusu picha hiyo
Mwandishi wa habari wa ITV Bw. Silvanus Kigomba akiuliza swali kwa Mzee Philip Mangula wakati wa mkutano huo. Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akifafanua zaidi swali la mwandishi huyo Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akielezea mambo mbalimbali
yanayohusu uchaguzi huo ambapo amesema CCM ni waumini wa Amani na kwamba
katika jimbo la Kalenga hagombei Godfrey Mgimwa bali kinachogombea ni
Chama cha Mapinduzi kwani ungekuwa ni ukoo wa mgimwa unagombea basi
ungeona akina mgimwa woote wako mbelea wakipiga debe ili washinde lakini
kwa sababu ni CCM inagombea ndiyo maana utaona viongozi na wana CCM
mbalimbali wakishiriki katika kampeni hizo ili kukipatia ushindi chama
chao. Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula akizungumza nabaadhi ya
viongozi wa CCM mkoa wa Iringa kabla ya kuelekea Ifunda ambako atapiga
kambi huko.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-IRINGA)
No comments:
Post a Comment