Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 3, 2014

Mashabiki Wa Al Ahly Wapewa Onyo La Kutoingia Uwanjani Siku ya Mechi ya Marudiano na Yanga.



 

Mamlaka za usalama nchini Egypt katika jiji la Cairo zimewaonya mashabiki wa Al Ahly kutoingia katika uwanja wa Cairo International stadium kuhudhuria mechi ya raundi ya pili ya CAF Champions league kati ya Al Ahly dhidi ya Young Africans S.C. itakayochezwa mnamo March 9.

Katika taarifa iliyotolewa jana Jumapili, polisi wa Cairo walisema kwamba itapambana na jaribio lolote la mashabiki kujaribu kuingia uwanjani.

Azmi Megahed, msemaji wa FA ya Misri, alisema raia hawatoruhusiwa kuhudhuria mechi hiyo kutokana na sababu za kiusalama.

Jumamosi wiki iliyopita, polisi walipambana na mashabiki wa Zamalek White Knights ambao walijaribu kuingia katika uwanja wa Huo kuangalia mchezo kati ya Zamalek dhidi ya mabingwa wa Angola Cabo Schrob. Fujo hizo zilipelekea kwa kukamatwa kwa mashabiki 33.

No comments:

Post a Comment