Maelfu ya
saini za mashabiki wa soka zimekusanywa katika ombi rasmi la kutaka
kiungo wa Manchester United Tom Cleverley kufungiwa kucheza katika
michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Brazil mwaka huu.
Mpaka sasa
ombi hilo limeshakusanya jumla ya saini 6,000 ndani ya kipindi cha masaa
36, lilikusanya saini 4,000 ndani ya masaa 24, na lilosomeka kama
ifuatavyo: 'Tom Cleverley, ambaye tayari ameshaichezea England mechi 13,
amekuwa akiteuliwa na Roy Hodgson katika vikosi vya England bila kuwa
na sifa yoyote ya maana.
'Tunaamini
katika taswira nzuri ya kikosi cha taifa hili kubwa na kwamba tunataka
azuiwe kushiriki katika michuano ijayo ya kombe la dunia.
'England
inaaminika kuwa ni timu mbovu katika michuano mikubwa, hivyo aibu zaidi
inaweza kuepukika kwa kutomjumuisha yeye na kiwango dhaifu kitachoshusha
jitihada za timu nzima.'
Kama ilivyo
kwa wachezaji wenzie wengi, Cleverley ameshindwa kurudia kiwango chake
kizuri alichokuwa nacho miaka miwili iliyopita, kilichomfanya Sir Alex
Ferguson kumuita 'special player'
Cleverley
amefunga goli moja tu katika michezo 32 aliyoichezea klabu yake na
amekuwa akisemwa mpaka na mashabiki wa timu yake, hasa kwenye mtandao wa
Twitter.
Pamoja na
kusemwa sana, kiungo huyo mwenye miaka 24 amechaguliwa na kocha Hodgson
alhamisi iliyopita kuunda kikosi cha Denmark wiki hii, na inaonekana ana
nafasi ya kwenda Brazil.
Chanzo:shaffihdauda.com
No comments:
Post a Comment