Mbunge
mteule wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akibebwa juu
na wanachama wa CCM huku wakiserebuka kusherekea ushindi katika ofisi
kuu ya CCM mkoa wa Iringa ambapo CCM imeshinda kwa mbali katika
matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika jana kwenye jimbo la Kalenga mkoni
Iringa, Tume ya taifa ya uchaguzi imemtangaza Godfrey Mgimwa kuwa
mshindi katika uchaguzi huo ambapo CCM imeshinda kwa kura 22962 huku
CHADEMA ikipata 5853 na chama cha CHAUSTA kura 150 Chama cha Mapinduzi
kimefanikiwa kushinda katika kata zote kumi na tatu za jimbo hilo.
Watu
wengi walijitokeza asubuhi kupiga kura na hali ilikuwa ni ya utulivu
kabisa na watu wengi waliopiga kura wameishukuru serikali na tume ya
uchaguzi kwa kuandaa utaratibu mzuri na kufanyika kwa uchaguzi wenye
utulivu..(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KAlENGA)Mbunge
mteule wa jimbo la Kalenga kupitia CCM Bw. Godfrey Mgimwa akipiga picha
na wanachama wa Chama cha Mapinduzi katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa
ambapo wana CCM walifurika kushangilia ushindi huo mnono ambao CCM
imeshinda kwa kishindo.
MATOKEO KAMILI HAYA HAPA
No comments:
Post a Comment