Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 31, 2014

MATUKIO YA BUNGE LA KATIBA LEO HAYA HAPA

 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Waziri Mkuu, Mstaafu, Edward  Lowassa (katikati), Andrew Dhenge (kulia) na James Mbatia   wakiteta, bungeni jini Dodoma machi 31,2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba na Maspika, Anne makinda wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (kushoto) na Pandu kificho wa Baraza la Wawakilishi wakiteta, Bungeni Mjini Dodoma Machi 31,  2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Zakia Meghji(kushoto) na Christopher Ole Sendeka(kulia) wakijadiliana leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika Kamati zao kwa ajili ya kuanza kupitia rasimu ya Katiba mpya.
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Anne Makinda (kushoto) na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Namelok Moringe Sokoine (kulia) wakibadilishana mawazo leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika vikao vya Kamati mbalimbali za kupitia vifungu mbalimbali rasimu ya Katiba mpya zoezi ambalo  limeanza leo .
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba James Lembeli (kushoto) na Mchungaji Peter Msigwa (kulia) wakijadiliana leo mjini Dodoma kabla ya kuelekea katika Kamati zao kwa ajili ya kuanza kupitia rasimu ya Katiba mpya.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta akiondoka katika ukumbi wa Bunge mara baada ya kuharisha kikao cha Bunge leo mjini Dodoma ambao wajumbe wameelekea katika Kamati zao mbalimbali kupitia vifungu vya rasimu ya Katiba Mpya.
Picha na Tiganya Vincent-Dodoma.
     

No comments:

Post a Comment