Wakuu
nchini Libya, wamesema kuwa wameikamata meli moja iliyokuwa na bendera
ya Korea Kaskazini, ikiwa na shehena haramu ya mafuta katika bandari
inayodhibitiwa na waasi.
Msemaji
wa shirika la kitaifa la mafuta, amesema kuwa meli hiyo ilisimamishwa
ilipokuwa ikijaribu kungoa nanga na kwa sasa inasindikizwa katika
bandari inayodhibitiwa na serikali ya Libya.
Maafisa
wa serikali ya Libya waliisimamisha Meli hiyo ya Korea Kaskazini
ilipokuwa ikiondoka kutoka bandari inayodhibitiwa na waasi siku ya
Jumatatu ikiwa imesheheni mzigo usio rasmi wa mafuta ghafi.
Jeshi la nchi hiyo limethibitisha tukio hilo.
Waasi wa
zamani wanaotaka kuitenga eneo la Libya Mashariki, wamekuwa wakimiliki
bandari ya Al-Sidra na vituo vingine muhimu vya kuuzia bidhaa nje katika
eneo hilo tangu Julai mwaka uliopita.
Mnamo
siku ya Jumamosi, walianza kupakia shehena ya mafuta yasiyosafishwa
ndani ya meli hiyo ya Korea Kaskazini iitwayo Morning Glory, iliyokuwa
imetia nanga katika bandari ya Al-Sidra.
Viongozi walaani wizi wa mafuta
Kiwanda cha mafuta nchini Libya
Siku ya
Jumatatu jeshi la wanamaji lilizuilia meli hiyo ilipokuwa ikiondoka
bandarini, huku amri ikitolewa ielekezwe hadi katika bandari
inayodhibitiwa na serikali.
Chama kikuu cha kisiasa nchini humo cha General National Congress, GNC, kimethibitisha kuzuiliwa kwa meli hiyo.
Runinga ya taifa Nchini Libya Al-Nabaa pia imeripoti tukio hilo kwa undani.
Walid
al-Tarhuni, ambaye ni msemaji wa zamani wa kundi la waasi ambalo
limekuwa likidhibiti bandari hiyo, ameiambia runinga ya Al-Nabaa kuwa
meli hiyo ya mizigo ilikuwa ikielekea katika bandari ya Zawiyah,
kilomita 50, Magharibi mwa mji mkuu Tripoli, kupakua mafuta hayo.
Utawala
wa Washington umesema kuwa umeshangazwa na tukio hilo na kukariri kuwa
mafuta inayotoka Libya ni mali ya raia wa nchi hiyo na wala sio ya
makundi fulani
No comments:
Post a Comment