Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 17, 2014

MESSI APIGA HAT-TRICK BARCELONA IKIIADHIBU OSASUNA 7 KWA BUYU

Messi amefunga hat-trick na kuisaidia Barcelona kuiangamiza bila huruma Osasuna na kupunguza pengo dhidi ya Real Madrid na Atletico Madrid katika kuelekea taji la La Liga.
Nyota wa Argentina Messi alianza kufungua karamu ya mabao kwa kufunga bao la kwanza kabla ya Alexis Sanchez kufunga bao la pili
 
Lionel .
Andres Iniesta akafunga bao kwa mkwaju wa yadi 25 na kuifanya Barca kwenda mapumziko wakiwa na mabao 3-0.
Magoli mawili zaidi ya Messi, na mawili ya Cristian Tello na Pedro, yaliihakikishia Barca ushindi na kufanya maandalizi makubwa kuelekea kwenye El Clasico dhidi ya Real Madrid jumapili ijayo.
Mabingwa watetezi Barca watasafiri hadi Bernabeu kuikabili Real Madrid wakijua kwamba wanahitaji kuwachapa vinara hao wa La Liga ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea taji lao la La Liga.
Vijana wa Gerardo Martino wako nyuma ya vinara Real kwa pointi nne na pointi moja nyuma ya Atletico huku ikibakia michezo 10 kumaliza ligi.

No comments:

Post a Comment