Mh
Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akitelemka katika moja
ya gari ambalo alilizindua kwa ishara ya kuzindua magari mengine yote
yatakayotumika kupambana na ujangili.
Mh Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akielekea kuongea na wanahabari baada ya uzinduzi huo
Haya ndiyo Magari ambayo yamezinduliwa Rasmi kwa ajili ya kupambana na majangili
Mh Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akizungumza na wanahabari
Picha zote na Maliasili zetu Blog
HII NDIO HOTUBA YAKE KAMILI
Ndugu Wanahabari:
Katika kutekeleza maazimio ya Bunge, na ahadi ya serikali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, leo nimekamilisha utaratibu wa kuzitoa silaha zilizokuwa chini ya TRA tangu mwezi wa Novemba mwaka 2012, ili kuzikabidhi kwa wapiganaji katika Hifadhi za Taifa, Mamlaka ya Ngorongoro, na Mapori ya Akiba kote nchini kwa lengo la kupambana na ujangili. Silaha hizi 500 aina ya AK47 ziligharimu jumla yaSh.427milioni kuzinunua, na leo Wizara yangu inatoa Shs.212 milioni kwa ajili ya kulipia kodi na ushuru mbalimbali ili Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA iziruhusu kutolewa.
Ndugu Wanahabari:
Kutokana na ukweli kwamba Pori ka Akiba la Selous lenye ukubwa wa kilometa za mraba 55,000 lina ukubwa unaokaribia Hifadhi zote za Taifa chini ya TANAPA ambazo zina ukubwa wa kilometa za mraba 57,000, na hivyo kulifanya Pori la Akiba la Selous kuwa kubwa mno ki-menejimenti na kiundeshaji, na ili kuweka mazingira wezeshi ya kupambana kikamilifu katika vita inayoendelea dhidi ya ujangili, leo nachukua hatua zifuatazo:
1. Nazipandisha hadhi Kanda 8 zilizopo Pori la Akiba la Selous ili ziweze
kujitegemea kiundeshaji (Semi Autonomous status), chini ya Mkuu wa kila Kanda
2.Naiagiza Idara ya Wanyamapori ikamilishe mchakato wa kufungua akaunti maalumu za benki kwa kila kanda ili kuwawezesha Wakuu wa Kanda hizi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
3. Mhifadhi Benson Kibonde ataendelea kuwa Meneja wa Pori lote la Selous kama ilivyo sasa na ataendelea kuwa msimamizi Mkuu wa Pori la Akiba la Selous, na atasaidiwa na Wakuu wa Kanda wafuatao:
- Msafiri Mashiku- Mkuu, Kanda ya Matambwe
- Asterius Ndunguru- Mkuu, Kanda ya Msolwa
- Adili Y. Zella- Mkuu, Kanda ya Liwale
- Bigilamungu Kagoma- Mkuu, Kanda ya Kingupira
- William Millya- Mkuu, Kanda ya Kalulu
- Munhu J. Ndunguru- Mkuu, Kanda ya Miguruwe
- Ramadhani Mkhofoy- Mkuu, Kanda ya Ilonga
- Msiba Kombo- Mkuu, Kanda ya Likuyu-Sekamaganga.
Wakati huo huo, tumechukua hatua za kuimarisha Kikosi Dhidi ya Ujangili KDU nchini zinazotekelezwa katika Kanda 8 nchi nzima na kuongozwa na Wakuu wa Kanda wafuatao:-
1. Paskal Mrina- Mkuu, Kanda ya Kaskazini-Arusha
2. Faustine Masalu- Mkuu, Kanda ya Mashariki- DSM
3. John Mbwiliza- Mkuu, Kanda ya Serengeti- Bunda
4. Benjamin Kijija- Mkuu, Kanda ya Ziwa- Mwanza
5. Charles Msilanga- Mkuu, Kanda ya Magharibi-Tabora
6. Keneth Sanga- Mkuu, Kanda ya Kati- Manyoni
7. Majid Lalu- Mkuu, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini-Iringa
8. Ibeid Mmari- Mkuu, Kanda ya Kusini- Songea.
Ndugu wanahabari:
Katika jitihada za kuimarisha ulinzi wa Tembo na mapambano dhidi ya Ujangili katika Pori la Akiba la Selous, tunawashukuru washirika wetu katika Uhifadhi, Frankfurt Zoological Society kwa kutupa Magari matano (5) aina ya Landrover. Nachukua nafasi hii kutangaza kuwa nagawa gari moja moja kwa Kanda zifuatazo ndani ya Pori la Akiba la Selous:
Kanda ya Matambwe
Kanda ya Msolwa
Kanda ya Kiwale
Kanda ya Kingupira
Kanda ya Kalulu.
Aidha, Mfuko wa Wanyamapori umenunua Magari 14 aina ya Toyota yenye thamani ya Shs.1.63 bilioni na nachukua nafasi hii kutangaza mgao wake kwenye Vituo vya Wanyamapori vifuatavyo:-
1.
Pori la Akiba Selous-Kanda ya Likuyu Sekamaganga -1
2.
Pori la Akiba Rungwa-2
3.
Pori la Akiba Uwanda-1
4.
Pori la Akiba Lukwati-PITI-1
5.
Pori la Akiba Kijereshi-1
6.
Pori la Akiba Rukwa-LWAFI-1
7.
Pori la Akiba Burigi-Biharamulo-Kimisi-1
8.
Pori la Akiba Lukwika-Lumesule-Msanjesi-1
9.
Pori la Akiba Moyowosi-Kigosi-1
10.
Pori la Akiba Maswa-1
11.
Pori la Akiba Mkungunero-1
12.
Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori PASIANSI-1
13.
Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori (TWPF)-1
Ndugu wanahabari:
Hapa Makao Makuu ya Wizara kunatokea mabadiliko yafuatayo:
1. Namteua Bw. Nurdin Chamuya, ambaye ni mwanahabari mzoefu, kuwa Msemaji wa Wizara ya Malisili na Utalii, na anachukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Bw.Chikambi Rumisha ambaye anarudi kwenye Idara yake ya Sera na Mipango.
Ndugu wanahabari,
Wizara ya Maliasili na Utalii inachukua hatua mahsusi kujenga uwezo wa watumishi wake na maaskari wanyamapori kupambana na kuushinda ujangili nchini. Nawaomba wananchi wote wajitolee taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa majangili kabla hawajaua Tembo na wanyama wengine. Tunamwomba kila raia awe sehemu ya mapambano dhidi ya ujangili. Tunaiomba jumuiya ya Kimataifa na washirika wetu wa naendeleo waungane nasi katika mapambani haya.
Tanzania Bila Ujangili Inawezekana.
Mungu ibariki Tanzania.
Asanteni
Lazaro Nyalandu, Mb.
WAZIRI
No comments:
Post a Comment