Mahakama
ya Misri imewahukumu wanachama 26 wa harakati ya Ikhwaanul Muslimiin ya
Misri adhabu ya kifo kwa tuhuma eti za kuvuruga umoja wa kitaifa na
kushambulia meli zinazopita katika mfereji wa Suez.
Mahakama
hiyo leo imewahukumu wanachama wa harakati hiyo ambao hawakuwepo
mahakamani, kwa tuhuma pia za kuanzisha na kuongoza mtandao wa kigaidi.
Mahakama hiyo imetangaza kuwa, wanachama hao wa Ikhwaanul Muslimiin watakabiliwa na adhabu ya kifo.
Mahakama hiyo imemhukumu pia mwanachama mwingine wa harakati hiyo adhabu ya kifungo cha miaka 15 jela.
Inafaa
kuashiria hapa kuwa, jeshi la Misri mwezi Julai mwaka uliopita
lilimuondoa madarakani kwa nguvu Muhammad Mursi rais aliyekuwa
amechaguliwa na wananchi na kisha kuwatia mbaroni viongozi waandamizi na
wanachama kadhaa wa harakati hiyo.
Wakati
huohuo, Waziri Mkuu wa serikali ya mpito ya Misri amekutana na Sheikh wa
al Azhar kwa shabaha ya kutafuta njia za kukabiliana na fikra za
kitakfiri.
Akizungumza
na Sheikh Ahmad Muhammad al Tayeb, Ibrahim Mahlab Waziri Mkuu wa Misri
ameisifu nafasi ya al Azhar katika kutoa mafunzo ya Kiislamu na
kusisitiza kuwa, Chuo Kikuu cha al Azhar kina uwezo mkubwa wa
kukabiliana na vitendo hivyo viovu kutokana na nafasi iliyokuwa nayo ya
kimaanawi.
Chanzo: kiswahili.irib.ir
No comments:
Post a Comment