


Aliyekuwa
Mwanachama wa Chadema kutoka kijiji cha Kamiyu na Katibu Mwenezi wa
Chadema kata ya Kamiyu akitangaza kuachana na Chadema na Kujiunga na CCM
hii leo kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Nzi.







Na.Baraka Kiwango.
Mbio
za Kampeni Jimbo la Kalenga zimendelea kushika kasi hii leo,Huku Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara Mh;Mwigulu Nchemba akiweka kambi kwenye Kata ya
Nzi kwa Muda wa masaa 10 na kufanya mikutano Minne siku ya leo kwenye
Vijiji vya Kipera,Kimayu,Nzi na Magubika.
Mwigulu
Nchemba mbali na Kumnadi Mgombea Wa CCM Kijana Godfrey William
Mgimwa,hii leo amevuna Wananchama Viongozi wa Chadema(Mwenyekiti kaya ya
Nzi,Katibu Mwenezi na Wanachama 73).Ambao kwa hiari yao wametangaza
kujiunga na Chama Cha Mapinduzi wakibeza hatua ya Chadema kuanza
kumkejeli Marehemu Mgimwa kuwa hakufanya kitu jimboni kwao ilihali
wamefikishiwa Umeme karibia asilimia 80 ya Vijiji vya Kalenga,Amejenga
Shule,Vituo Vya Afya na Visima vya maji.Pia haohao Chadema kwenye Msiba
walisikika kwenye Vyombo vya habari wakikili kuwa Marehemu Mzee Mgimwa
alikuwa kiongozi wa Mfano na Utendaji wake ulitukuka kwa Kalenga na
Taifa hili.
Katika
hatua Nyingine Mh:Mwigulu Nchemba ameendelea kusisitiza kampeni
zifanyike kwa amani na kila chama kina nafasi ya kujenga hoja kuhusu
kile watakachokifanya kwe Wanakalenga na sio Matusi.CCM tunajambo la
kuzungumza kuhusu Kalenga kwasababu ndio wenye Ilani inayotekelezwa hapa
Kalenga na ndio wenye Serikali iliyopo Madarakani,Kinachofanyika hapa
ni kumpa kura za ndio Kijana wetu Godfrey Mgimwa akamalizie Utekelezaji
wa Ilani ya CCM na Shughuli za Maendeleo alizoacha Marehemu Mgimwa kwa
Wanakalenga,Alisema Mwigulu.
No comments:
Post a Comment