Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, March 3, 2014

Pistorius akana mashitaka

 

Mwanaridha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amekanusha mashitaka ya kumuua mpenzi wake wakati kesi yake ikianza mjini Pretoria.
Pistorius ambaye ana ulemavu wa miguu na ambaye hutumia miguu bandia ameshitakiwa kwa kumuua mpenzi wake na mwanamitindo Reeva Steenkamp.
Oscar amesema alimpiga risasi marehemu kimakosa kwani alidhani alikua mwizi.
Mahakama mjini Pretoria ilimuachilia Pistorius kwa dhamana ya randi millioni moja, sawa na kiasi ya Dola laki moja.
Pistorius anasema kuwa alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya akidhani alikuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yake. Mauaji yake yalitokea siku ya Valentines mwaka jana.
Wiki jana mashirika ya habari za michezo, yalipata idhini ya kupeperusha kesi ya Pistorius moja kwa moja kutoka mahakamani.

No comments:

Post a Comment