Rais
Jakaya Kikwete wa pili kushoto akipata maelezo kuhusu msaada wa magari
11 kutoka kwa Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya
Afrika, Robert Muir (katikati)na kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini
Hans Koeppel katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Msaada huo umetolewa na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya
ujangili katika hifadhi za Serengeti Selous na Maswa. Mkurugenzi wa
Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert
Muir(katikati) akitoa hotuba yake kuhusu msaada magari 11 waliyoyatoa
kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za
Serengeti ,Selous na Maswa,kushoto wa pili ni Rais Jakaya Kikwete na wa
kwanza ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel na kulia wa
pili Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.
Rais
Jakaya Kikwete wa pili kushoto akionesha moja ya ufunguo wa msaada wa
magari 11 mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Frankfurt
Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir ( kulia wanne)
katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo
umetolewa na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika
hifadhi za Serengeti ,Selous na Maswa.
Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel akizungumza jamabo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kushukuru msaada magari 11
ulioyatolewa na Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda
ya Afrika, Robert Muir kwa ajili ya kupambana na vitendo vya
ujangili katika hifadhi za Serengeti, Selous na Maswa.
Picha na Magreth Kinabo -MAELEZO
No comments:
Post a Comment