
Kaimu
Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Neema
Rusibayila, akifungua rasmi warsha ya mradi wa upatikanaji na
utekelezaji wa pamoja kati ya Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP)
na Shirika la Kimataifa lisilokuwa la Kiserikali (NGO) PATH kwenye sekta
ya Afya katika utumiaji na uanzishwaji wa Teknolojia mpya katika
kupamba na magonjwa ya TB, Malaria na magonjwa yaliyoachwa katika nchi
za joto. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mkazi, Oparesheni wa UNDP, Bw.
Titus Osundina.

Washiriki
wakifuatilia mada mbalimbali katika warsha hiyo ya siku moja ambayo
ilikuwa inazungumzia mradi wa pamoja wa upatikanaji na utekelezaji kati
ya UNDP na PATH jinsi ya uanzishwaji wa Teknolojia mpya katika kupamba
na magonjwa ambayo yanapatikana katika nchi za joto.



Mgeni
rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt.
Neema Rusibayila akiteta jambo na Naibu Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Bw.
Titus Osundina wakati wa warsha ya Upatikanaji na Utekelezaji wa pamoja
katika miradi ya utathimini na mipango inayowashirikisha UNDP na PATH.

Picha
juu na chini ni Kaimu Mkurugenzi wa Kinga, Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii Dkt. Neema Rusibayila, akibadilishana mawazo na kusalimiana na
baadhi ya washiriki wa warsha hiyo.

No comments:
Post a Comment