Na: Mwandishi wetu, Dodoma
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba ,Mhe Samweli Sitta, amesikitishwa na kitendo cha baadhi ya
wanasiasa kujipanga kuvuruga mchakato wa katiba kwa kuweka misimamo ya kuleta
fujo Bungeni badala ya kujadili mambo kwa hoja.
Mhe. Sitta amesema hayo wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari mjini Dodoma
mara baada ya kuairishwa kwa kikao cha Bunge hilo jioni ili kutoa ufafanuzi wa
masuala mbalimbali yaliojitokeza Bungeni Jana.
Ukiwa na Habari au matukio tutumie kupitia namba yetu ya
Whatssap 0713966552 au email address sekdavid64@hotmail.com
“Tumekuwa tukipata taarifa ya vikao vya
wana UKAWA ambao wao wamejikita katika kukwamisha mchakato huu na kuazimia
kuleta vurugu kwa madai ya kumshinikiza mwenyekiti kuvunja kamati ya Uongozi.
Jambo hili si la kiungwana kwa kuwa kamati hiyo haikuchaguliwa na Mwenyekiti,
wao kama walitaka nafasi hizo wangegombea huko kwenye kamati zo kama
alivyojitokeza Mhe. Lipumba” alisema Mhe. Sitta
Pamoja na hilo, Mhe. Sitta anasema yote
yanayojitokeza hivi sasa ni mpango mahususi amabao katika nukuu za wanaukawa
walinukuliwa wakisema “lazima kieleweke,
Kamati ya Uongozi lazima ifumuliwe, na wajumbe wa kuteuliwa wote lazima watoke
UKAWA la sivyo hatuondoki Bungeni mpaka kieleweke”
Haya ni baadhi ya maazimio ya wanaukawa
ambao hawawaonei huruma wananchi waliwatuma kufanya kazi hii hapa Bungeni ya
Kuandika Katiba bora bali wameazimia kushinikiza maslahi yao binafsi kwa lengo
la kukwamisha mchakato mzima bila kujali kuwa serikali inatumia fedha nyingi
sana.
Akielezea hoja iliyoletwa na Lissu
aliyekuwa ameaomba mwongozo kulalamika kufanyika kwa mabadiliko ya vifungu
mbalimbali vya kanuni, Mhe. Sitta alisema
maelezo aliyoyaleta Lissu Bungeni
na kumtuhumu moja kwamoja, ni kuwahisha agenda jambo ambalo halikuwemo
katika orodha ya shughuli za Bunge Maalum kwa siku ya leo. Pamoja na hilo, Mhe.
Sitta alisema utaratibu huo ni wakawaida na hufanyika katika mabunge mbalimbali
kwa lengo la kuboresha kanuni kulingana na mahitaji yaliyopo na hususani kulingana
na mazingira wakati wowote.
Kuhusu utaratibu unaotumika, Mhe. Sitta alisema
kwa mujibu wa kanuni ya 58(i )na 59 inamruhusu
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na
Haki za Bunge Maalum kuwasilisha mapendekezo ya Mabadiliko ya Kanuni kama
yalivyofanyiwa na kamati hiyo Bungeni.
“Suala la kufanya marekebisho ya kanuni
swala la kikanuni ni jambo ambalo Mhe. Kificho alikuwa awasilishe Bungeni,
lakini kwa kuwa wajumbe walikuwa wanahamu na miongozo nikaona niwape nafasi,
lakini cha kushangaza wakaanza kujadili jambo ambalo bado halijawasilishwa
Bungeni”
Akiomba mwongozo wake leo jioni, Mhe.
Lissu alipinga jedwali la marekebisho ambalo hata hivyo halikuwa limewasilishwa
rasmi Bungeni hivyo kuleta hoja yake kuleta vurugu na kusababisha Bunge
kuhairishwa. Kimsingi swala la kujadili jambo ambalo halijawasilishwa Bungeni
ni kinyume na matakwa ya kanuni.
Kuhusu vipolo vya kanuni ya 37 na 38, Mhe
Sitta amesema tayari kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum imelifanyia kazi
na lipo katika taarifa iliyokuwa iwasilishwe na Mwenyekiti wa Kamati hiyo.
“kwa kuwa tulikuwa na taarifa za vurugu
hizo, niliona ni bora niruhusu miongozo ili yote yaelekezwe kwangu kuliko
mwenyekiti wa Kamati hiyo kuzomewa kwa jambo ambalo amelifanya kikanuni, na
kesho kanuni hizi zitaletwa tena Bungeni pamoja na mapendekezo mengine” alisema
Mhe Sitta.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za
Bunge Maalum ni Mhe. Pandu Amer Kificho na kesho anatarajia kuwasilisha taarifa
ya kamati yake kwa mujibu wa ratiba iliyopo ambapo Bunge litaendelea tena saa
kumi jioni.
No comments:
Post a Comment