Basi
la Hood linalofanya safari zake kutoka Arusha kwenda Mbeya, namba za
usajili T.488 AXV aiana ya Scania imepata ajali mbaya leo, majira ya saa
3 asubuhi na kusababisha kifo cha Mtu mmoja na kujeruhi wengine 16.
Ajali
hiyo imetokea katika, barabara ya Same - Mwanga, Kijiji cha Kiverenge
wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo taarifa za awali zinasema kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi ya mbele.
Kamanda
wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo ambapo amesema katika ajali hiyo alifariki Abiria mmoja aliyemtaja
kwa jina la Joshua Likumbia, Raia wa Kenya, ambaye alikuwa akisafiri
kuelekea jijini Mbeya.
Kamanda
Boaz amesema majeruhi katika ajali hiyo ambao ni 16, akiwemo dereva wa
Basi, Fadhili Hashim wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na
Hospitali ya Rufaa mkoani Kilimanjaro, KCMC.
Kamanda
Boaz ameendelea kufafanua kuwa majeruhi hao nane wamelazwa Same huku
wengine 8 wakikimbizwa mjini Moshi katika hospitali ya KCMC kutokana na
hali zao kuwa mbaya ambapo watatu kati yao wakia wamelazwa katika chumba
cha wagonjwa mahututi.
No comments:
Post a Comment