Daraja la Kigamboni limekamilika kwa zaidi ya asilimia arobaini na tano na matumaini makubwa ya kumalizika kwa ujenzi huo kwa muda uliopangwa Julai mwakani yakionekana huku nyumba zilizokuwa zinazuia ujenzi huko zikibomolewa kwa nguvu na serikali.
Akizungumza
na ITV jijini Dar es Salaam meneja mradi huo injinia Karim Mattaka
amesema ujenzi huo umeshaanza kuleta matumaini makubwa kutokana na nguzo
mbili zilizokuwa zinakwamisha kuwa tayari na zoezi linaloendelea ni
kuhamisha maji katika maeneo yalinayochimbiwa nguzo hizo sambamba na
kuchimbia nguzo kubwa za kupokea baraja hilo upande wa barabara ya
Mandela.
Aidha
injinia Karimu amejaribu kufafanua mfumo wa barabara na daraja hilo
namna utakavyotumika baada ya kukamilika na kuwahakikishia watanzania
ujenzi huo utakamilika kwa wakata kama mambo yataenda kama
yalivyopangwa.
Mwenyekiti
serikali ya mtaa wa Vijibweni Bw. Athman Ally akielezea kuhusiana na
hatua iliyochukuliwa na serikali ya kuvunja nyumba za baadhi ya wakazi
waliogomea fidia amesema wao walipewa taarifa na mwanasheria mkuu na
baadaye akatakiwa kwenda kusimamia zoezi la uvunjaji wa nyumba hizo.CHANZO ITV
No comments:
Post a Comment