Timu
ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania kutoka Kituo cha Mwanza imeondoka leo
(Machi 26 mwaka huu) kwenda Brazil kushiriki mashindano ya Kombe la
Dunia kwa Watoto wa Mitaani.
John
Kadutu ambaye ni mjumbe wa Bodi ya kituo hicho, na pia mjumbe wa Mkutano
Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) akiwakilisha klabu
za Mkoa wa Mwanza ndiye kiongozi wa msafara wa timu hiyo ya Tanzania.
Michuano
hiyo ya siku 10 inayoshirikisha watoto wa mitaa (wavulana na wasichana)
inaanza keshokutwa (Machi 28 mwaka huu). Nchi 19 zinashiriki michuano
hiyo itakayofanyika katika Jiji la Rio de Janeiro.
Mbali
ya Tanzania, nchi nyingine zinazoshiriki michuano hiyo kwa upande wa
wavulana ni Argentina, Burundi, India, Kenya, Liberia, Marekani,
Mauritius, Misri na Pakistan. Kwa wasichana ni Afrika Kusini, Brazil, El
Salvador, Indonesia, Msumbiji, Nicaragua, Philippines, Uingereza na
Zimbabwe.
Mwaka 2010 mashindano hayo yalifanyika Durban, Afrika Kusini ambapo pia Tanzania ilishiriki.
MABINGWA WA MIKOA WATAKIWA MACHI 30
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linavikumbusha vyama vya mpira wa
miguu vya mikoa kuwa vinatakiwa kuwasilisha majina ya mabingwa wao
kufikia Machi 30 mwaka huu.
Majina
ya mabingwa yanatakiwa kuwasilishwa pamoja na usajili wa wachezaji
waliotumika kwenye ligi ya mkoa. Kila klabu inaruhusiwa kuongeza
wachezaji watano kutoka ndani ya mkoa husika, ambapo unatakiwa
uthibitisho wa usajili huo.
Mpaka
sasa ni vyama viwili tu ndivyo vimeshawasilisha mabingwa wao. Vyama
hivyo ni Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Pwani (COREFA) ambapo bingwa
wake ni Kiluvya United, na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Lindi
(LIREFA) ambapo bingwa ni Kariakoo SC.
Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer
Tanzania Football Federation (TFF).
No comments:
Post a Comment