Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 12, 2014

UPDATES: KIVUKO CHA MV. MAGOGONI CHAPATA TATIZO LA GHAFLA USIKU HUU



 Taarifa ya Uhakika iliyotufikia hivi punde kwenye mtandao huu ,inaeleza kuwa Kivuko cha Mv. Magogoni kinachovusha watu na mali zao kutoka Magogoni - Kigamboni jijini Dar es Salaam, kimepatwa na tatizo jioni hii baada ya kukatika kwa sehemu ya mkono unaoshika mlango wa upande mmoja wa kuvushia magari na waenda kwa miguu.Utaratibu wa kutengeneza Kivuko hicho unafanywa hivi sasa na Mafundi wa Kivuko huku Abiria wakiwa wamesimama pembeni kusubiria utaratibu mwingine.
Sehemu ya Abiria waliokuwa kwenye kivuko hicho wakiwa wamesimama pembeni kusubiria Kivuko kingine.

No comments:

Post a Comment