MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP),
Eliezer Feleshi, amemfungulia shtaka jipya la kuua kwa kukusudia, mmiliki wa
jengo la Ghorofa 16 lilioanguka Mtaa wa Indira Ghandi Jijini Dar es Salaam na
kusababisha maafa ya watu (27) waliosadikiwa kufukiwa na kifusi cha ghorofa
hilo Machi 28, mwaka jana.
Feleshi amethibitisha kuwa washtakiwa hao wamefunguliwa shtaka jipya leo Jumatano
Machi 12, mwaka huu, Katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu la kuua kwa
kukusudia.
“Ninachojua ni kuwa kesi hiyo
inaondolewa na kuwa substated with another kesi, kwa hiyo mashtaka ya awali
yameondolewa yameunganishwa na mashtaka mapya ya mauaji ya kuua kwa kukusudia,
tunasubiri kukamilika kwa upelelezi” alisema Feleshi.
Alisema hapo awali mshtakiwa huyo
(Raza Hussein Raza) akiwa na wenzake alikuwa anakabiliwa na shtaka la kuua bila
kukusudia lakini baada ya upande wa Serikali kugundua mambo mengine sasa
mmiliki huyo atakabiliwa na Shtaka la kuua bila kukusudia.
Kwa mujibu wa Sheria za Nchi, kesi
za mauaji haina dhamana kutokana na ukubwa wa tukio ambapo Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu haina uwezo wa kushughulikia kesi hiyo.
Kutokana na Sheria hiyo Hakimu wa Mahakama hiyo Devota Kisoka ameamuru watuhumiwa hao kupelekwa gerezani ili kusubiri Sheria kufuata mkondo wake, ambapo DPP anadaiwa kutofuata kipengele hicho.
Kutokana na Sheria hiyo Hakimu wa Mahakama hiyo Devota Kisoka ameamuru watuhumiwa hao kupelekwa gerezani ili kusubiri Sheria kufuata mkondo wake, ambapo DPP anadaiwa kutofuata kipengele hicho.
Jengo hilo lililokuwa likijengwa
mkabala na Msikiti wa Shia Ithnasheri ulioko Barabara ya Indira Gandhi na Kampuni
ya ‘Lucky Construction Limited’ ambapo lilianguka majira ya saa 2.30 asubuhi
Machi 28, mwaka jana, wakati ujenzi ukiendelea juu huku chini ya jingo hilo
shughuli za kibinadamu zikiendelea
Shughuli mbalimbali katikati ya eneo
hilo zilisimama kwa siku nzima baada ya jengo hilo kuanguka na kusababisha vifo
vya watu (27), na wengine kuokolewa
No comments:
Post a Comment