Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, March 5, 2014

URUSI YASEMA HAIJAPELEKA MAJESHI UKRAINE

 
Rais Vladimir Putin wa Urusi, amesema bado hakuna haja kwa nchi yake kupeleka majeshi nchini Ukraine. 
Bwana Putin amesema Urusi ina haki ya kutumia njia zote kulinda raia wake walioko mashariki mwa Ukraine.
Amekanusha taarifa kwamba majeshi ya Urusi yamewazingira raia wa Ukraine walioko katika jimbo la Crimea, bali ni watu wanaoiunga mkono Urusi na ambao wanajilinda wenyewe.
Bwana Putin amesema kuondolewa madarakani kwa Rais Viktor Yanukovych katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev ni "ukiukaji wa katiba na uporaji wa madaraka kijeshi.".
Amesema wapiganaji hao wameitumbukiza Ukraine katika "vurugu". Pia amesema wapigania utaifa na wapinga usemiti wanarandaranda katika mitaa ya Kiev na miji mingine.
Amesema iwapo watu wanaozungumza Kirusi mashariki mwa Ukraine watahitaji msaada wa Urusi, basi Urusi itakubaliana na ombi lao.
"kama tutaona hali hii ikianza kutokea maeneo ya mashariki, tuna haki ya kutumia kila njia" amesema.
Bwana Putini amesema katika jimbo la Crimea watu wenye silaha wanaoiunga mkono Urusi na raia wamezingira kambi za kijeshi za Ukraine, sio askari wa Urusi.
"Majeshi ya eneo hilo kwa ajili ya kujilinda" ndiyo yanayohusika na kuchukuliwa kwa majengo ya serikali katika Crimea, amesema.
Viktor Yanukovych rais wa Ukraine aliyepinduliwa
Ukraine imesema Urusi imepeleka maelfu ya askari katika eneo la Crimea hivi karibuni.
Uhasama umeongezeka katika kituo cha kijeshi cha Belbek karibu na Sevastopol, mji wa bandari ambao ni kambi ya majeshi ya majini ya Urusi.
Akizungumzia kupinduliwa kwa Bwana Yanukovych, Bwana Putin amesema kiongozi huyo aliyeondolewa madarakani nchini Ukraine alikubali matakwa yote ya wapinzani.
Bwana Putin amesisitiza kuwa Bwana Yanukovych bado ni rais halali wa Ukraine.
Amesema kuna mambo matatu ya kumwondoa madarakani rais, ameyataja kuwa ni kifo, kujiuzulu au kushtakiwa.
Bwana Yanukovych alikimbilia Urusi, na Bwana Putin aliwaambia waandishi wa habari: "Sifikiri kama ana mustakabhali mwema kisiasa".
Urusi ilimsaidia kwa sababu za "kibinadamu", amesema, "vinginevyo angekuwa ameuawa".

No comments:

Post a Comment