skip to main |
skip to sidebar
UVUTAJI WA SIGARA NA MATOKEO YAKE KWA WATOTO
Uvutaji sigara unaathiri afya ya kina mama wajawazito.
Utafiti mpya kutoka ulaya na marekani
kazkazini unasema kuwa,kupigwa marufuku kwa uvutaji wa sigara hadharani
kumesababisha kushuka kwa viwango vya wanawake kujifungua mapema kabla
ya mda wao kwa asilimia 10.
Idadi ya watoto waliolazwa hospitalini
kutokana na ugonjwa wa pumu pia imepungua kwa asilimia 10% katika
maeneo ambayo uvutaji sigara hadharani umepigwa marufuku kulingana na
wanasayansi kutoka chuo cha Edinburgh nchini Scotland.
Mmoja ya waanzilishi wa utafiti huo
Prof Aziz Sheikh ambaye ripoti ya utafiti wake imechapishwa katika
jarida la matibabu duniani Lancet,anasema kuwa mataifa yasio na marufuku
hiyo yanapaswa kutilia maanani matokeo hayo kwaajili ya kizazi chao cha
baadaye.
Kwa sasa ,sheria dhidi ya uvutaji sigara zinaathiri asilimia 16 ya idadi ya watu dunaini.
Chanzo, bbcswahili (R.M
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI ZAIDI.
No comments:
Post a Comment