CHANZO CHA UGONJWA
Andrea anayeishi kwa mateso makali maeneo ya Argentina, Manzese jijini Dar, anasema mwaka 2005 akiwa anafanya kazi katika mashine ya kusaga na kukoboa, alijikuta akianza kuumwa na vidole vya mguu wa kulia na baadaye maumivu hayo kuhamia kiunoni, kitu kilichomfanya kukosa raha.
Anaendelea kusimulia: “Mara baada ya kusikia maumivu ya vidole na kiuno, nilikwenda katika Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

“Nilipofika huko, wakaamua kuchukua vipimo vya damu kwa ajili ya
uchunguzi lakini hawakutaka kunipa majibu, nilishangaza sana kwa sababu
sijawahi kuona kitu kama hicho.
KUFIWA NA MKE
“Mwaka 2006 nilifiwa na mke wangu, Nuru Kassim ambaye ameniachia mtoto mdogo, Agness mwenye umri wa miaka 7. Hilo lilikuwa pigo kubwa kwangu.
“Mwaka 2006 nilifiwa na mke wangu, Nuru Kassim ambaye ameniachia mtoto mdogo, Agness mwenye umri wa miaka 7. Hilo lilikuwa pigo kubwa kwangu.
“Kutokana na matatizo ya kuugua nilishindwa kumlea mtoto wangu hasa
ikizingatiwa kuwa sikuwa nafanya kazi, bahati nzuri mwanamke mmoja wa
Kiarabu alijitokeza na kuamua kumchukua Agness na kuishi naye,” alisema
Andrea kwa masikitiko.
Aliongeza kuwa aliendelea kupata matibabu japokuwa hayakubadilisha
kitu chochote zaidi ya mguu wake kuanza kuota magamba ambayo yaliufanya
kubadilika na kufanana na mti uliokauka. Baada ya kuona hali imekuwa
hivyo na maumivu yakimzidia kila siku, aliamua kurudi Hospitali ya
Mwananyamala ambapo walimwambia achukuliwe vipimo kwa mara nyingine.
KUHAMISHIWA MUHIMBILI
“Kilichofanyika ni kuchukuliwa vipimo kwa kutumia kipimo cha kupimia saratani ya ngozi ambacho hujulikana kitaalamu kama Biopsy na hivyo kukutwa na ugonjwa wa kansa ya ngozi uitwao Kaposis Sarcoma,” alisema.

Alisema hakuweza kupatiwa matibabu zaidi ya kuandikiwa karatasi ya kuhamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar.
Alipokuwa Muhimbili, Andrea alilazwa kwa muda wa miezi miwili bure
kutokana na kutokuwa na uwezo kifedha, madaktari waliliangalia tatizo
lake kiundani na wakashauri asikatwe mguu hivyo wakamuandikia dozi ya
dawa za vidonge na kumruhusu kurudi nyumbani.
Mpaka sasa Andrea anaendelea na vidonge hivyo na hana msaada wowote
zaidi ya kutembea mtaani na kuomba chochote japo apate chakula cha siku
na anashindwa kurudi hospitali kwa kuwa hana hata senti tano.
Andrea anaomba msaada kwa yeyote aliyeguswa na habari hii ili aweze
kupata fedha za kuendeleza matibabu yake na kujikimu. Kutoa ni moyo na
ukimsaidia utapata baraka za Mungu. Unaweza kuwasiliana naye kupitia
namba ya dada yake. Zainabu John Kimweri – 0656 037075.
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGIIII
BOFYA HAPA NA ULIKE PAGE YETU KWA HABARI NYINGIIII
No comments:
Post a Comment