Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Jeshi la Magereza, Deonice Chamulesile akiwaongoza Mamia ya Waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho kwa Marehemu Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo aliyefariki kwa ajali ya gari Aprili 22, 2014 majira ya saa Saba mchana wakati akisindikiza Mahabusu kutoka Mahakama ya Mwanzo Kimanzichana Wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani. Katika ajali hiyo pia walikufa Mahabusu wanne waliokuwa wanatoka kusikiliza kesi zao.Baadhi ya Askari wa Jeshi la Magereza wakiaga mwili wa Marehemu Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo katika Kambi ya Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam leo Aprili 24, 2014.
Mke wa Marehemu Sajini wa Magereza, Peter Shelukindo akisaidiwa na mmoja wa Waombolezaji kumuaga Mme wake aliyefariki kwa ajali ya gari.
Mmoja wa ndugu wa Marehemu akiwa amebebwa na Waombolezaji baada ya kuzimia katika tukio la kuaga mwili wa Marehemu Sajini wa Magereza Peter Shelukindo.
Baadhi ya Waombolezaji walijitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Sajini wa Magereza Peter Shelukindo aliyekufa kwa ajali ya gari Wilayani Mkuranga(wa kwanza kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.

No comments:
Post a Comment