Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, April 18, 2014

BARCA NI SHIDA! NEYMAR, ALBA NJE WIKI NNE!!

388904_heroa 
MAJANGA BARCA!. Mshambuliaji wao raia wa Brazil, Neymar ataa nje ya uwanja wa wiki nne, wakati naye beki Jordi Alba atakaa muda kama huo baada ya wote kupata majeruhi.
Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa Neymar alipata majeruhi ya mguu jana katika mchezo wa fainali ya kombe la Mfalme dhidi ya Real Madrid.
Kinda huyo mwenye miaka 21 alishindwa kuisaidia Barca kuepukana na kipigo cha mabao 2-1, huku Mbrazil huyo akikosa nafasi ya wazi dakika za lala salama.
Neymar atakosa mechi zijazo dhidi ya Athletic Bilbao, Villarreal, Getafe na Elche.
Hata hivyo klabu ya Barca ina matumaini kuwa nyota wake huyo anaweza kurudi katika mechi ya mwisho dhidi ya Atletico Madrid.Na Baraka Mpenja

No comments:

Post a Comment