Afisa wa polisi akilinda mojawapo ya maeneo katika jiji la Nairobi ambalo usalama wake unatatiza.Bomu linaripotiwa kulipuka kwenye gari na kuuwa watu wanne ikiwa ni Polisi wawili na abiria wawili ambao wanashukiwa walikuwa na bomu hilo kwenye gari karibu na kituo cha Polisi cha Pangani.
Lakini ilivyotokea inaripotiwa na gazeti la Starndard kwamba Polisi hao wawili waliwakamata washukiwa waliokuwa na kuamua kuwapeleka kituo cha Polisi wakiwa na bomu hilo kwenye gari!
Kabla ya kufika kituoni bomu hilo lilipuka na kuuwa wote Polisi pamoja na washukiwa ambao walikuwa kwenye jaribio la kujitoa muhanga.Haijajulikana mara moja kwanini Polisi hao waliamua kuchukua hatua ya namna hii lakini habari zaidi baadaye..
Watu wanne, wakiwemo maafisa wawili wa polisi, wameuawa jana usiku mjini Nairobi baada ya gari walilolizuia kulipuka, lilipokuwa likielekea katika kituo cha polisi katika eneo la Pangani, jijini Nairobi.
Maafisa wa polisi wanasema wanajaribu kuitambua miili ya washukiwa hao.
No comments:
Post a Comment