Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, April 9, 2014

Je unamiliki gari aina ya Toyota Rav4 ama Camry ? Kampuni ya Toyota imeagiza magari aina 6 yaregeshwa kutokana na hitilafu zifuatazo.


Toyota yaagiza magari milioni 6.5 kurejeshwa viwandani

Kampuni kubwa ya uundaji na uuzaji wa magari ya Japan, Toyota i meagiza magari milioni sita unusu kurejeshwa ilikufanyiwa ukarabati kutokana na upungufu mbalimbali.
Idadi hiyo ya kurejeshwa magari ni kubwa mno kurejeshwa viwandani.
Kampuni hiyo kubwa zaidi duniani ya uundaji magari inarejesha magari aina ya Yaris, Urban Cruiser, RAV4 na Hilux.
Kuna hitilafu katika kifuko cha hewa cha kumlinda dereva -(air bag) katika jumla ya magari milioni tatu, ikiwa haiwezi kuchomoka ili kimlinda dereva wakati wa ajali.
Aidha kuna hitilafu pia katika baadhi ya viti, usukani na kifaa cha mota ya kuwasha magari.
Kampuni ya Toyota inasema haijabaini ni ajali ngapi, majeruhi au maafa ambayo yamesababishwa na matatizo hayo yaliyogundulika majuzi.
Jumla ya magari 20,000 yanahitilafu ya mota ya kuwasha .
Mwezi Februari , Toyota iliagiza magari milioni 1.9 aina ya Prius hybrid yaregeshwe kutokana na hitlafu iliyopelekea magari hayo kupoteza mwendo ghafla.
Kwa Jumla magari milioni 25 yamearegeshwa katika kipindi cha miaka miwili u nusu iliyopita .CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment