Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwaonyesha wanafunzi kutoka chuo cha Whitworth Marekani bango la linaloonyesha wajumbe wa Kamati Kuu wa CCM wakati wa mkutano kati yake na wanafunzi hao waliomtembelea Makao Makuu ya Chama Ofisi Ndogo Lumumba.
Wanafunzi wa Chuo cha Whitworth wakisoma bango lenye kuonyesha wajumbe wa kamati kuu ya CCM wakati wa mkutano wao na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambapo walipata nafasi ya kujifunza mambo mengi na mazuri ya Chama Cha Mapinduzi kushoto ni Mwalim Grace Valentine wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere.
Profesa John C.Yoder (kulia) akiandika mambo muhimu ya Chama Cha Mapinduzi pamoja na wanafunzi wake wakati wa kikao na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ,wanafunzi hao walipata kuelezwa historia ya chama,muundo wa chama, historia ya muungano na mambo mengine mengi yanayohusu siasa za Chama Cha Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment