Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 24, 2014

PICHA MBALIMBALI ZA MATUKIO YA BUNGE MAALUM LA KATIBA

 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili katika eneo la Ukumbi wa Mkutano leo mjini Dodoma kwa ajili ya kuendelea na mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya. 
 . Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mkutano wakifuatilia  mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya leo mjini Dodoma.

  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Goodluck Joseph Ole-Medeye akitoa mchango wake akiwasilisha  katika Ukumbi wa Mkutano  mjini Dodoma wakati wa mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya. 
  Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta(kulia) na Mjumbe wa Bunge hilo Profesa Costa Mahalu(kushoto) wakijadiliana kitu  mjini Dodoma wakati wa mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya..
 Baadhi ya Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakibadilishana mawazo ndani ya Ukumbi wa Mkutano wakifuatilia  mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta (kushoto mstari wa kwanza) wakijadiliana kitu  mjini Dodoma na Wajumbe wa Bunge hilo Mwingulu Nchemba(katikati) na Dkt. Asha-Rose Migoro(kulia) wakati wa mjadala wa sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya.

 
 Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba Dkt. Fennella Mukangara (kushoto) na Profesa Mark Mwandosya wakibadilishana mawazo  mjini Dodoma wakati wa mapumziko ya mkutano ulikuwa ukijadili sura ya kwanza na sita ya rasimu ya Katiba mpya. 
 Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta (kushoto ), Makamu wake Samia Suluhu Hassan( wa pili kulia) , Mjumbe wa Bunge hilo Adam Malima(kulia) na Mwandishi wa Kitabu cha Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha , Minael-Hosanna O. Mdundo(wa pili kushoto) wakibadilishana mawazo mara baada ya kuwakabidhi nakala ya kitabu hicho viongozi hao  mjini Dodoma.
 Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samia Suluhu Hassan (kulia ) wakijadiliana kitu na Mwandishi wa Kitabu cha Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha , Minael-Hosanna O. Mdundo( kushoto)  mjini Dodoma.
 Mwandishi wa Kitabu cha Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha , Minael-Hosanna O. Mdundo( kulia) akiwaonyesha Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta(kushoto) na Makamu wake Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwaelezea maudhui ya Kitabu chake leo mjini Dodoma.
 Mwandishi wa Kitabu cha Masimulizi ya Sheikh Thabit Kombo Jecha , Minael-Hosanna O. Mdundo( kulia) akimkabidhi nakala ya Kitabu chake Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta(kushoto) mjini Dodoma. Mwingine ni Makamu wake Samia Suluhu Hassan (katikati).  

No comments:

Post a Comment