Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, April 10, 2014

SOMA WARAKA WA JULIUS MTATIRO KUHUSU TOVUTI YA TUME YA KATIBA


KAMA VITA IMEFIKIA HAPA, WAJUMBE WA 
TUME YA KATIBA WAJIHADHARI

Serikali isiyo na soni. Imefunga tovuti ya tume 

ya mabadiliko ya katiba, eti lengo kuu ni 
kuhakikisha wananchi hawapati rejea na 
nyaraka mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia 
uelewa na ufahamu wao. Sababu ya serikali ni 
kuwa, kazi ya tume imekwisha hivyo na tovuto 
yake haina kazi

Serikali inayoogopa wananchi wake wasiendelee 

kuelimika, kujielimisha na kufahamu mambo muhimu 
ya nchi ni serikali ya ajabu sana.

Tovuti ni maktaba za kielektroniki, tume ya katiba 

ya Kenya hadi leo tovuti yao ipo hewani, tume ya katiba 
ya Ghana hadi leo inafanya kazi, ya Afrika ya kusini 
hadi sasa iko hewani baada ya miaka mingi ya 
kutunga katiba ya taifa hilo mara baada ya Madiba 
kuingia madarakani.
Hapa Tanzania, serikali iloituma tume kukusanya maoni 

ya wananchi sasa imekasirika, kwa hiyo inayapiga 
vita maoni ya wananchi, inaipiga vita tume ya 
mabadiliko ya katiba. Serikali nyingi za kiafrika zina 
rekodi mbaya mno kila inapotokea matakwa yake 
fulani yamezuiwa na na watu fulani kwa njia halali.

Kwa chuki hizi za waziwazi dhidi ya tume na Wajumbe 

wa tume ya mabadiliko ya katiba, natoa wito kwa 
wajumbe hao kuwa makini na nyendo zao na 
kutojiamini sana. Ikumbukwe nchi hii watu 
wamewahi kung'olewa macho na wengine 
meno na vyombo vya dola viliishia 
kukamata wendawazimu na kuwapa mashtaka 
huku wahusika halisi waliotumwa kufanya kazi hizo 
za kinyama kwa maslahi tusiyoyajua wakitamba 
mitaani hadi leo.

Nasisitiza kuwa, ikiwa serikali ya kiafrika inafunga 

hadi tovuti yenye taarifa za maoni ya wananchi 
iliyokuwa wazi kwa umma, ni muhimu wajumbe wa 
tume wakajichunga sana. Mimi siiamini sana serikali 
hii ambayo leo inaweza kukutuma kazi na kesho 
asubuhi ikakugeuka na kukupiga vita wewe na 
kazi uliyoifanya.

Haya ni maoni na mtizamo wangu binafsi. Inatosha 

tu kuheshimu mawazo ya kila mtu.

No comments:

Post a Comment