
Waasi nchini Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa unasema kuwa
vikosi vinavyoipinga serikali nchini Sudan Kusini viliwaua mamia ya watu
kwa sababu ya kabila lao wakati vilipouteka mji wa Bentiu wiki jana.
Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, watu hao
walilengwa wakiwa katika maeneo salama walikokuwa wanahifadhiwa kama
vile msikitini, makanisani na hospitalini.Watu wa kabila laNuer, ni wafuasi wakubwa wa kiongozi wa waasi na makamu wa zamani wa Rais Riek Machar
Wapiganaji wanaomuunga mkono makamu wa rais wa zamani Riek Machar waliuteka mji wa Bentiu ambao ni mji mkuu wa jimbo la Unity siku sita zilizopita.
Walinda amani wa Umoja wa Mataifa walilaani kile walichokitaja kama mauaji yanayowalenga raia kwa misingi ya ukabila.
Rais Salva Kiir anatoka kabila la Dinka ambalo ndilo kabila kubwa kuliko yote nchini Sudan Kusini
Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu ambao hawakuwa wa kabila la Nuer,waliuawa Bentiu.chanzo Bbc
No comments:
Post a Comment