Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, April 21, 2014

Wakazi wa kijiji cha Ng’ong’ona mkoani Dodoma wanakabiliwa na tatizo la maji hali inayopelekea kufuata huduma ya maji vijiji vya jirani.



Akizungumza na Dodoma fm mwenyekiti wa kijiji cha ng’ong’ona bwana Venansi Kisumuni  amethibitisha kuwepo kwa tatizo hilo na kukiri kuwa  maji ni tatizo kubwa hivyo wanalazimika kutumia maji ya korongoni kwa matumizi ya nyumbani.
Nae bi Suzani matonya mkazi wa ngogona  amesema kuwa  amekuwa akiteseka  tangu utoto mpaka leo hajafanikiwa kupata maji mbali na kutozwa michango mbali mbali kwa ajili ya huduma hiyo hivyo kuiomba  selikali iwasaidie kupata huduma ya maji.
Bwana venance amehitimisha kwa kusema kuwa kwa sasa wanalazimika kununua  maji kwa sh mia tatu hadi miato kutoka kwenye makaro hali inayo wawia vigumu kulingana na hali ya uchumi.Na Dodoma Fm

No comments:

Post a Comment