Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwasili katika Ukumbi wa Mikutano kwa ajili ya kuendelea kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba Mpya mjini DodomaWauguzi na Waganga wa Zahanati ya Bunge mjini Dodoma wakitoa msaada wa huduma ya kwanza na kufanya maandalizi ya kumpeleka Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ziana Mohamed Haji katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma leo baada ya kupata matatizo ya mshutuko.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ambapo pia ni Ndugu na Jamaa wa Mjumbe wa Bunge hilo Ziana Mohamed Haji wakijadiliana na watendaji wa Bunge hilo jinsi ya kumsaidia baada ya kupata matatizo ya mshutuko mjini Dodoma. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Balozi Seif Ally Idd(katikati) akibadilishana mawazo na Wajumbe wa Bunge hilo Mohamed Aboud Mohamed(kushoto) na Haji Omar Heri (kulia) mjini Dodoma wakati mapumziko mafupi ya mjadala kuhusu Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba mpya.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mizengo Pinda (kulia) akibadilishana mawazo na Wajumbe wenzake Mohamed Aboud Mohamed(katikati) na Dkt. Tereza Huvisa(kushoto) mjini Dodoma wakati wa mapumziko mafupi ya kujadili Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba mpya. Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Saada Mkuya Salum akichangia maoni yake leo mjini Dodoma kuhusu Sura ya Kwanza na Sita ya rasimu ya Katiba mpya.
Picha na Ofisi ya Bunge Maalum la Katiba
No comments:
Post a Comment