Simba nao watashuka dimbani wakiwa na mahesabu magumu zaidi ya kujihami kutokubali kufungwa mao mengi au kama yale walioyowafungwa watani wao ama kutokea kile kilichotokea katika mechi ya nani mtani Jembe kwa kuanza kufungwa na kisha kufanya kazi ya kusawazisha.
Japo mchezo wa kesho hautakuwa na mvuto kama ambavyo timu hizo zingekuwa zinagombea nani atwae ubingwa na nani awe mshindi wa pili, lakini bado mechi hiyo itakuwa ni ngumu na si kama ambavyo wengi wanaifikiria kuwa itakuwa ni rahisi na hasa kama unavyojuwa pindi wanapokutana watani wa jadi.chanzo Kajunason Blog

No comments:
Post a Comment