Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, May 21, 2014

17 wauawa katika shambulizi Borno,Nigeria



Watu 17 wameuawa katika shambulizi lililofanywa dhidi ya kijiji kimoja Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Mji wa Alagarno ambao uko katika jimbo la Borno, uko karibu na mji wa Chibok ambako wasichana zaidi ya miambili walitekwa nyara na kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram wiki tano zilizopita.
Hili ni shambulizi la hivi karibuni kufanywa nchini Nigeria wakati nchi hiyo ikikumbwa na kitendawili cha kuwatafuta zaidi ya wasichana miambili waliotekwa nyara na Boko Haram.
Juhudi hizo zinawashikirisha wataalamu wa ujasusi wa kimataifa kutoka Israel, Marekani na Uingereza.
Pia limetokea siku moja tu baada ya milipuko miwili kutokea mjini Jos katika jimbo la Plateau ambapo takriban watu 118 waliuawa Jumanne usiku.
Juhudi za kuwatafuta maiti bado zinaendelea.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa shambulizi lililofanyika mjini Jos, lilisababishwa na Boko Haram na kwamba huenda ni ujumbe kwa serikali kuwa wapiganaji hao wanaweza kushambulia wakati wowote wanapotaka.CHANZO BBC

No comments:

Post a Comment