Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania anayeichezea klabu ya
TP Mazembe ya DR Congo, Mbwana Ally Samatta yuko hatihati kuichezea timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars katika mchezo wa marudiano kesho kutwa
(jumapili) dhidi ya Zimbabwe, mjini Harare,
kuwania kupangwa hatua ya makundi kusaka tiketi ya kushiriki kombe la
mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
Taarifa za uhakika ni kwamba Samatta alipata majeruhi ya
nyama za paja katika mechi ya ligi ya mabingwa barani Afrika mei 25 mwaka huu
dhidi ya wapinzani wao AS Vita mjini Lubumbashi, huku akifunga bao pekee katika
ushindi wa TP Mazembe wa bao 1-0. Katika mchezo huo, Samatta alitolewa dakika ya
75 kutokana na majeruhi hayo.
Hata hivyo imeelezwa kuwa shirikisho la soka Tanzania, TFF,
baada ya kuambiwa na TP Mazembe kuwa Samatta ni majeruhi, wao walilazimisha
kumtumia mchezaji huyo.
Ili kusoma mahojiano yote yaliyofanyika baina ya mwandishi
na meneja wa Samatta bofyawww.bkmtata.blogspot.com
No comments:
Post a Comment