Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, May 1, 2014

HABARI YA KUSIKITISHA::KIGOGO WA USALAMA WA TAIFA AULIWA KINYAMA DAR!!


Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.


Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

No comments:

Post a Comment