1. Paul Pogba-kiungo wa
Ufaransa, miaka 21.
kwa msaada wa Mtandao
Pogba
akiwa bado ana miaka 21 amekuwa jasiri ndani na nje ya uwanja. Wengi
walishangaa kumuona kiungo huyo akipanda kiwango chake kwa kasi alipoondoka
Manchester United na kujiunga na Juventus mwaka 2012 kwa lengo ka kutafuta
namba katika kikosi cha kwanza.
Amekuwa
shujaa wa Claudio Marchisio katika
sehemu ya kiungo kwenye ligi ya Seria A msimu
uliopita na aliichezea Ufaransa mechi ya kwanza ya kirafiki ya kimataifa machi
2013 dhidi ya Georgia.
Mwezi
Julia mwaka huo huo alifanya kazi kubwa kuisaidia timu ya taifa ya Ufaransa
chini ya miaka 20 katika fainali za kombe la dunia, haikuwa rahisi kwa Ufaransa
kwenda kombe la dunia bili kijana huyu mahiri.
Umahiri
wa Pogba amempatia nafasi ya kucheza timu ya taifa na taarifa nzuri ni kwamba
atakuwa huru nchini Brazil kutoa mchango wake kama alivyofanya nchini Italia.
Kuwepo kwa Yohan Cabaye na Blaise Matuidi katika safu ya kiungo kutamruhusu
Pogba kusogea mbele safu ya ushambiliaji.
Frederic
Lipka, ambaye ni mkurugenzi wa kituo kilichomlea Pogba cha Le Havre kabla ya kwenda
England, alisema mwaka 2010 kuwa kijana
huyo yuko vizuri kiufundi kuliko hata Patrick Vieira wakati akiwa na umri kama
wake. Kwasasa tunasubiri kuona alimaanisha nini.
2. Joel Veltman- Beki wa
kati wa Uholanzi, miaka 22.
Habari
njema kwa beki huyu wa Ajax ni kwamba; kocha mkuu wa Uholanzi Van Gaal ameamua
kumpa nafasi katika kikosi chake kinachotumia mfumo wa 4-3-3.
Van
Gaal alimpa nafasi ya kuichezea Uholanzi kwa mara ya kwanza katika suluhu ya bila
kufungana na Colombia mwezi novemba mwaka jana.
Veltman
ni mchezaji kijana wa Ajax, lakini hajulikani kirahisi. Namna anavyocheza na
kimiliki mpira, uwezo wa kupiga mashuti na pasi ndefu kunaonesha kama amekaa
muda mrefu katika kikosi hicho. Kiukweli alicheza mechi yake ya kwanza wiki
chache baada ya msimu wa ligi kuu wa 2011-2014 kuanza na kutulia zaidi. Katika
msimu mzima amejiimarisha na kuwa chaguo la kwanza la Ajax.
Siku
si nyingi anaweza kufanya hayo kwa taifa lake, Mfumo wa kulinda kuanzia safu ya
ulinzi unaopendelea Van Gaal unahitaji
wachezaji wanaobadilika na kuweza kuusoma mchezo na kucheza vizuri. Hii kazi
yote ni ya Veltman na anaimudu vizuri.
Pia
Van Gaal anapenda kuona mpira unakwenda
mbele. Kwa maana hiyo Veltman anaonekana
ndiye chaguo sahihi kuelekea fainali za kombe la dunia mwaka huu. Tusubiri
kuona beki huyu atafanya nini?.
3.
Bernard, Kiungo wa Brazil, miaka 21.
Kwa bei yake ya paundi milioni 25, Bernard
alizikimbiza timu nyingi wakati akiwa katika klabu yake ya Atletico Mineiro
mwaka jana. Lakini Shakhtar Donetsk walijikaza kisabuni na kuinasa saini ya
kiungo huyo majira ya kiangazi mwaka jana. Walimpokea vizuri na kuikarimu sana
familia yake baada ya kuwasili Ukraine. Licha ya Bernard kuzoea kwa taratibu
maisha ya soka nje ya Marekani kusini, Shakhtar wanaamini jitihada zao za
kumnasa zilizaa matunda.
Bernard anacheza mpira wa kasi, anapenda kutanua
uwanja kulia na kuingia eneo la namba 10. Mpaka sasa ameanza mechi tatu tu za
kimataifa kati ya 10 alizocheza , na anaonekana atatumika pia msimu huu wa
kombe la dunia.
Mbali na wengi kumdharau kwa urefu wake wa futi 5
na inchi 6 na uzito wa kilo 63, Bernard amekuwa akionesha kiwango cha ajabu.
“Shakhtar hawataki kuniachia kwa sssa.” Alionya katika mahojiano ya karibuni na
O Globo baada ya Asernal na Tottenham kutangaza
tena nia ya kumtaka .
Sasa tunasubiri kuona maajabu yake katika fainali
za kombe la dunia mwaka huu katika ardhi yake.
4. Mattia Destro –mshambuliaji
wa Italia, miaka 23.
Mambo yalienda tofauti kidogo. Destro angeletwa katika ulimwengu wa soka na José
Mourinho.
Alikuwa mfungaji wake wakati Mourinho akiwa Milan.
Mshambuliaji huyo alikuwa katika kikosi kilichotwaa ubingwa wa UEFA, hata kama
hakucheza mechi yoyote.
Baada ya Mourinho kuondoka, Destro aliuzwa katika
klabu ya Genoa, japokuwa alianza kuongeza kasi ya kiwango chake baada ya
kujiunga na Siena mwaka 2011.
Kiwango chake kiliwavutia zaidi Roma na kumsajili
kwa dau zuri-lakini kuingia kwa kocha Rudi Garcia katika klabu hiyo kumemweka
katika kiwango kikubwa zaidi na kuiteka dunia.
Destro amekuwa mshambuliaji bora anayesifiwa na
kocha wake, huku akimuelezea kama “mshambuliaji aliyekamilika”. Hakuna utata wa
namba kwake. Katikati ya mwezi aprili
mwaka huu alifunga bao lake la 13 katika
ligi ya seria A, huku magoli yake mengi akifunga dakika za mwisho za 85 kwenye
michezo mingi. Kwasasa kwenye ligi kubwa barani Ulaya hakuna mwenye rekodi ya mabao ya
aina hiyo.
Destro anafunga
kila aina ya goli: amekuwa akipiga mashuti ya mbali na karibu. Anaweza kuwa
chaguo la kwanza katika fainali za kombe la dunia, lakini kiwango chake
kitamuokoa kwasababu ana upinzani mkubwa kutoka kwa Pablo Daniel Osvaldo.
5. William Carvalho ,
kiungo wa Ureno miaka 21
Sporting Clube de Portugal ni akademi kubwa kwa
soka la vijana, lakini William Carvalho ni ushahidi kuwa baada ya kituo hicho kuwakuza nyota wakubwa,
Cristiano Ronaldo na Luis Figo, sasa kinamleta nyota huyo mwenye miaka 21 anayeonekana
kuwa kiungo bora zaidi wa Ulinzi na amekuwa na kiwango kikubwa mno katika klabu
ya Lisbon baada ya kurudi katika klabu hiyo akitokea katika mkataba mrefu wa
mkopo kwenye klabu ya Cercle Brudgge.
Kujituma na kuwajibiki wa Carvalho kulimfanya
apewe nafasi ya kucheza kwa mara ya kwanza katika mechi ya “play-off” kuwania kombe la dunia dhidi ya Sweden mwezi
novemba mwaka jana.
Pia alicheza kwa dakika zote dhidi ya Cameroon
mwezi machi mwaka huu katika mechi ya kimataifa ya kirafiki na kujihakikishia
namba katika kikosi cha kwanza.
Jambo jema kwa kocha Paulo Bento ni kuwa nyota wa Porto, Fernando, mzaliwa wa Brazil, tayari
amepata kibali cha kuichezea Ureno, lakini kutokea kwa Carvalho kunaweza
kumfanya asimuhitaji tena.
Manchester United wamekuwa katika mawindo ya
kumnasa Carvalho na ada inayotajwa ni paundi milioni 30. Bento ni kocha mwenye
maamuzi magumu, haitashangaza kuona anamuanzisha Carvalho katika mchezo wa
ufunguzi wa kombe la dunia dhidi ya Ujerumani.
6. Mario Götze-kiungo
mshambuliaji wa Ujerumani, miaka 21.
Ni
mchezaji ambaye aliwashitua wengi baada ya kutolewa tangazo mwezi aprili 2013
kuwa anaondoka Borussia Dortmund na
kujiunga na wapinzani wao Bayern Munich. Mashabiki wa Dortmund waliumia sana
kwasababu waliamini nyota huyo kijana angekuwa msaada mkubwa kwa Jurgen Klopp.
Inawezekana
Gotze aliondoka kwa sababu ya presha ya kutaka kuvunja rekodi ya kuwa mchezaji
ghali zaidi kijana kuwahi kutokea nchini Ujerumani akiwa na miaka 21. Dau la
paundi milioni 37 lilikuwa kubwa sana kwake. Mashabiki walichukizwa na kitendo
cha yeye kuondoka, lakini maslahi ndio ilikuwa sababu .
Gotze
ni mtulivu ndani na nje ya uwanja, na alidhihirisha hilo baada ya kufunga bao
la kuongoza la Bayern Munich aliporejea katika uwanja wake wa Signal Iduna Park
dhidi ya timu yake ya zamani ya Dortmund mwezi novemba mwaka jana.
Kwenye
mashindano makubwa ya karibuni, Ujerumani wameshindwa kuonesha cheche kali na mwaka
huu wanahitaji `wauaji` wakali, matarajio yao yapo kwa Gotze mwaka huu.
Wanategemea miujiza yake ya soka, uwezo wake wa kupiga chenga na kasi yake ya
`umeme` na uwezo wa kufunga vinawapa matumaini makubwa sana Ujerumani.
Hii
ilionekana wakati alipofunga bao moja la mwisho katika mechi ya kimataifa ya
kirafiki dhidi ya Chile baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Mesut Ozil,
ikiwa ni bao lake la saba . Wengi wanaamini nyota wa Asernal, Ozil atakuwa
msaada mkubwa kumpikia mambo Gotze ambaye kuanza kwake katika kikosi cha Bayern
Munich msimu uliopita kulimweka matatani Frank Ribery. Ujerumani wana bahati ya
kuwa na mchezaji muhimu kama yeye. Ngoja tusubiri kuona atafanya nini Brazil
mwezi ujao.
7.
Aleksandr
Kokorin, Mshambuliaji wa Urusi, miaka 23
Huyu ni kijana mwenye miaka 23 anayekiongoza
kizazi cha soka la Urusi kwa sasa. Ni rafiki wa vyombo vya habari,
anashirikiana na anapatikana mara nyingi-lakini mbali ya hayo hapo juu ana
kipaji kikubwa mno cha soka. Anzhi kwasasa wanafikiria kumuuza kwa paundi
milioni 19, lakini wanamuuza moja kwa moja katika klabu yake ya zamani ya
Dinamo Moscow kabla ya kucheza mechi yake ya kwanza.
Kokorin ni mchezaji mwenye akili ya mpira, mjanja
na amekuwa mmaliziaji mzuri msimu wa karibuni. Aliifungia Urusi baadhi ya mabao
muhimu yaliyowapa tiketi ya kwenda Brazil (alifunga mabao manne katika mechi
saba alizoanza).
Urusi chini ya Fabio Capello wapo kundi moja na
Ubelgiji, Algeria na Korea kusini na watapata faida ya kumtumia nyota huyu
mwenye kipaji cha juu.
Urusi wanaamini kuwa nyota huyu atakuwa na
ushirikiano mkubwa na mzoefu Aleksandr Kerzhakov katika safu ya ushambuliaji.
Hii ilionekana wazi katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ambayo Urusi
ilishinda dhidi ya Armenia mwezi machi mwaka huu. Hakuna kingine zaidi ya Urusi
kusubiri furaha kutoka kwa kijana huyu.
8. Mateo Kovacic, kiungo
wa Croatia, miaka 19
Ili kudhihirisha kuwa Croatia imebarikiwa kuwa na viungo mafundi kama Luka Modric Robert Prosinecki na Zvonimir Boban, sasa Mateo
Kovacic mwenye miaka 19 ni ujio mpya katika kikosi cha nchi hiyo na atacheza
pamoja na mafundi wengine.
Inahitaji ushahidi? anauliza mwalimu wake wa mpira
aliyemkuza Niko Kranjcar, wakati huo huo naye Boban alikiri kuwa kijana huyo atakuwa mzuri zaidi
yake enzi za nyuma.
Kumbuka Inter walikubali kumnunua kwa dau la
paundi milioni 15 kutoka Dinamo Zagreb januari mwaka 2013. Makocha wote wawili
wa timu hizi alizocheza wamehangaika kupata namba yake halali uwanjani. Kovacic
amepewe jezi namba 10 ya Wesley Sneijder, na hii inatokana na jinsi Inter
wanavyomthamini wa kipaji chake.
Hajaonesha kiwango kikubwa sana katika taifa lake,
lakini kijana huyo aliisaidia nchi yake kushinda dhidi ya Serbia kuwania kufuzu
kombe la dunia akicheza kama kiungo wa ulinzi, lakini alionesha soka safi
kwenye mechi ya “play-off” na Iceland, ambapo alifunga bao kwa kupiga chenga
hatari. Sasa Brazil inamsubiri.
9.
Eden Hazard , kiungo mshambuliaji wa
Ubelgiji,miaka 23
Hazard amekuwa na kiwango cha juu katika klabu ya
Chelsea hata zaidi ya alivyokuwa katika klabu ya Lille kwenye msimu wake wa
mwisho. Ameongeza matumaini makubwa katika nchi yake kuelekea kombe la dunia na
inaelezwa kuwa hayuko peke yake katika kambi ya Ubelji, wapo wachezaji wengi wenye
kiwango kikubwa na morali kama yeye.
Hazard amekuwa na safari ndefu. Sasa anataka
mafanikio zaidi akianza kuitumikia Ubelgiji kwenye fainali za kombe la dunia
kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 23 ikiwa ni miaka karibu mitatu imepita tangu
alipoichezea nchi yake mechi ya kwanza dhidi ya Kazakhstan kuwania kucheza fainali ya Euro 2012.
Kwasasa hakuna shaka kabisa juu ya kuanza kwake
katika kikosi cha Ubelgiji. Hazard amekuwa akifanya kazi nzuri kutoka winga ya
kushoto na katikati, japokuwa kufunga mabao
mawili tu wakati wa kutafuta tiketi ya kufuzu kombe la dunia
kulisababisha akosolewe. Lakini bado amedhihirisha uwezo wake akiwa na Chelsea
ambapo hakuwa na kizuizi tena cha kufunga. Kama Hazard ataonesha kiwango kama hicho
katika kombe la dunia, basi tunatarajia Ubelgiji iwe tishio.
10.
ackson Martinez, mshambuliaji wa Colombia,
miaka 27
Hakuna mtu nchini Colombia asiyetarajia kuona
Radamel Falcao anaimarika zaidi kuelekea kombe la dunia baada ya kupata
majeruhi makubwa ya goti, lakini hata kama atapona, bado atahitaji msaidizi
wake.
Mbali ya Falcao kuhitaji watu wa kumrithi akiwemo
nyota wa Hertha Berlin, Adrian Ramos na Teufilo
Gutierrez wa River Plate, Jackson Martinez ndiye mwenye nafasi kubwa. Akiwa
amerithi jezi namba 9 ya Falcao katika klabu ya Porto, Jackson amefanya makubwa
zaidi kama nyota huyo mwenzake wa kimataifa, akifunga magoli 41 katika mechi 53
alizoanza akiwa na Porto tangu alipojiunga na klabu hiyo kutokea klabu ya Jaguares mwaka 2012.
Labda tuseme anatakiwa kuambiwa juu ya kuzingatia
wajibu wake wa kimataifa. Martinez alianza katika mechi nne tu za kuwania
kufuzu kombe la dunia na hakufunga bao lolote. Lakini msimu huu ana njia ndefu
baada ya kupewa hadhi ya kusimama mbele akiwapiku Fredy Guarin na James
Rodriguez.
Jackson amekuwa na umbo zuri na uwezo wake wa
kufunga sio siri. Amefunga mabao muhimu kwa Porto katika mechi za ligi na
kimataifa. Nyota huyo mwenye miaka 27 anaweza kuwa msaada mkubwa kwa Colombia
na kurithi mambo ya Falcao ambaye hatakuwa fiti sana kutokana na majeruhi.
No comments:
Post a Comment