Mzungu huyo ambaye jina tunalihifadhi, alidaiwa kufanya
tukio hilo la kinyama Mei 26, mwaka huu na inadaiwa Aneth alipomkatalia,
alimtimua nyumbani hapo kwa kumtupia virago.
Chanzo makini kilidai kuwa, baada ya kutupiwa virago bila
kupewa mshahara wake sambamba na kipigo, Aneth aliripoti tukio hilo katika
Kituo Kidogo cha Polisi cha Tabata, Dar na muda mfupi polisi walifika nyumbani
hapo lakini Mzungu huyo hakutoka ndani, akakataa kuzungumza chochote
Taarifa zilidai kuwa, baada ya polisi kukutana na kizingiti
hicho, walimpigia simu kiongozi wao ambaye aliwaamuru warudi kituoni wajipange
upya.
Akisimulia zaidi ishu hiyo, Aneth alisema polisi
walipoondoka eneo hilo, umati uliochukizwa na kitendo hicho ulikusanyika nje ya
nyumba ili kumdhibiti ‘mtasha’ huyo kwa lolote.
Kuna jirani mmoja
alipiga simu tena kituo cha polisi alipoona hali ya hewa imechafuka ndipo
polisi wakafika kwa mara nyingine na difenda na kufanikiwa kuingia ndani kwa
kutumia geti kubwa, walipofika walikuta milango imefungwa lakini ilisemekana
aliruka ukuta na kutimkia kusikojulikana.
Polisi waliniambia
nimpigie simu ajisalimishe lakini nilipompigia alisema hayupo na kama
tunamhitaji tukutane sehemu huku na yeye akiwa na polisi wake
kilisema chanzo.
Mmiliki wa nyumba hiyo anayeishi Kigamboni, Mr. Cris alipoulizwa
kuhusiana na ishu hiyo, alikiri kupokea malalamiko na manyanyaso kutoka kwa
Aneth.
Akisimulia zaidi maisha anayoishi na Mzungu huyo, Aneth
alisema:
Alikuwa
akinitafutia sababu za kunitimua kwani hivi karibuni kwa bahati mbaya
nilipoteza ufunguo wa ndani, akanipiga mateke na kunisababishia maumivu makali
mwilini kiasi cha kushindwa kutembea.
Lakini lililoniuma
zaidi ni hili la kunilazimisha eti nifanye mapenzi na mbwa wake, amekuwa
akifanya hivyo mara kwa mara mimi nikaona siyo sawa na nilipokataa ndipo
yakanikuta hayo.
Aneth aliripoti matukio hayo katika Kituo Kidogo cha Polisi
Tabata na kupewa fomu ya matibabu (PF-3) sambamba na kufunguliwa jalada la kesi
namba TBT/RB/3132/2014/ SHAMBULIO na jalada la uchunguzi lenye namba
TBT/IR/1829/2014/UCHUNGUZI.
No comments:
Post a Comment