Ujumbe wa Tanzania ukiinua bendera juu kuashiria uwepo wao mkutanoni.
Ujumbe wa Tanzania (waliovaa sare za kijani), kutokakushoto Kanali Martin BusungunaLuteniKanali Joseph Bakariwakati wa mkutano.
Kanali Busungu akipiga kura wakati wa uchaguzi wa viongozi wapya ya Baraza.
Luteni Kanali Bakari akichangia mada wakati wa Mkutano.
Na LuteniKanali Juma Sipe (PA, Marekani).
JWTZ limeshirikiMkutano wa
Baraza la Michezo la Kimataifa (General Assembly and Congress of the
International Military Sports Council -CISM) uliofanyikaMjini Quito,
EquadoAmerica ya Kusinikuanziatarehe 05-09 Mei, 2014.
Mkutano huo ulijadilina kuendelea
kusikiliza na ushiriki wa majeshi katika Michezo ya Kimataifa chini ya
Kauli mbiu ya Baraza hilo isemayo Urafiki kupitia Michezo
(Friendship through sports), msisitizo ukiwa katika kutumia michezo kama
chombo cha kueneza amani na utulivu kati ya mataifa duniani. Badala ya
kukutana na kushirikiana katika maeneo ya vita na migogoro, majeshi
yakutane katika michezo na kujenga uelewano na mashirikiano
yatakayopunguza uwezekano wa kuingia katika vita kama njia ya kutatua
migogoro.
Moja ya mambo yaliyojitokeza
katika mkutano huo ni pamoja na ushiriki mdogo wa nchi za Afrika
ikilinganishwa na mabara mengine, uliodaiwa kutokana na kukosekana
fedha, mwamko mdogo wa viongozi wa majeshi ya nchi husika na kutoona
umuhimu wa kujenga mahusiano kupitia michezo.
Aidha, Mkutano ulimchagua Rais
mpya wa Baraza hilo, Kanali Abdul Hakeem kutoka Bahrain na Kanali Dorah
Mumby (Guinea) kuwa Katibu Mkuu wa kwanza kutoka Afrika.
Ushiriki wa Tanzania na
utekelezaji wa maazimio ya CISM umekuwa wa mfano kwa miaka kadha sasa.
Kwa mfano,katika mkutano wake wa mwaka 2008 uliofanyika Paramaribo,
Suriname, Meja Joseph Bakari (sasa Luteni Kanali) alitunukiwa na Bodi ya
Wakurugenzi ya Baraza hilo Nishani iitwayo ‘Order of Grand Knight’ kwa mchango wake uliopelekea kuanzishwa kwa “Twalipo Youth Sports Foundation” (twalipo soccer academy.blogspot. com) nchini Tanzania.
Katika mkutano huojumla ya
wanachama 76 walihudhuria kati ya wanachama 104 wa Baraza hilo. Tanzania
iliwakilishwa na Kanali MartinBusungu, Mkurugenzi wa Utimamu wa Mwili,
Michezo na Utamaduni kutoka Makao Makuu ya Jeshi na LuteniKanali Joseph
Bakari, Afisa mnadhimu kutoka Kurugenzi hiyo.
Mkutano huo wa mwaka hutanguliwa
na mikutano ya kimabara (Afrika, Ulaya, AsianaAmerika) ambako masuala ya
michezo ya Majeshi yanayogusa mabara husika hujadiliwa.
Kutoka ukanda wa Afrika Mashariki
na Jumuiya ya ushirikiano Kusini mwa Afrika nchi zilizoshiriki ni pamoja
na Kenya, Uganda na Zambia.
Kwa uelewa zaidi tafadhali tembelea wavuti www.cismmilsport.org
No comments:
Post a Comment