Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, May 17, 2014

KING'AMUZI CHA STER TIMES CHAUA MTU CHUNYA-MBEYA



Mtu mmoja Joseph Admin [35] mkazi wa kijiji cha Matundasi wilaya ya Chunya aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi wakitumia silaha za jadi fimbo,mawe na marungu.
Tukio hilo limetokea tarehe jana majira ya saa nne usiku katika ofisi ya kijiji cha Matundasi, kata ya Matundasi tarafa ya kiwanja wilaya ya Chunya. 
Kundi hilo la wananchi wakiongozwa na fabiani john na thobias asukenye walivunja mlango wa ofisi hiyo na kuanza kumshambulia marehemu ambaye alikuwa amekamatwa pamoja na mwenzake Abbas Jumanne [29] kwa tuhuma za kuiba ving’amuzi viwili vya Star Times Chunya mjini ambavyo walikutwa navyo. 
Hata hivyo polisi walifika eneo hilo mara baada ya kupata taarifa za vurugu hizo na kufanikiwa kumuokoa mtuhumiwa Abbas Jumanne. Watuhumiwa Fabian John na Thomas Asukenye walikimbia wao na wenzao wengine walioshiriki katika mauaji hayo wanatafutwa wakamatwe.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anaendelea kutoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria, badala yake wahakikishe wanawafikisha katika mamlaka husika watuhumiwa wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali ili hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe. 
Lakini pia watu wenye tabia ya kufanya uhalifu waache kwani itapunguza uwezekano wa kushambuliwa na wananchi wanaojichukulia sheria mikononi.

No comments:

Post a Comment