Wamiliki, madereva na abiria wote mnatangaziwa kuwa kituo
cha daladala Mwenge kitafungwa rasmi siku ya Jumapili jioni tarehe 01.06.2014.
Kuanzia siku ya jumatatu asubuhi tarehe 02.06.2014 kituo kitakachokuwa
kinatumika ni Makumbusho tu.
Sababu kubwa ya kufunga kituo hicho ni ufinyu wa eneo hilo
jambo linalochangia dadalada kushindwa kuingia kituoni kwa wakati hasa vipindi
vya asubuhi na jioni hivyo kusababaisha foleni kubwa katika eneo la Mwenge.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa eneo hilo kwa sasa
litabaki kuwa eneo la wazi.
Madereva mnatakiwa kutii agizo hili ili kuepukana na hatua
kali ambazo zitachukuliwa dhidi ya yeyote ambae atakaidi, aidha abiria
mnatakiwa msilazimishe kushushwa eneo ambalo hakuna kituo cha daladala.
Barabara za kuingia na kutoka kituoni Makumbusho zinaendelea
kukarabatiwa na Manispaa ya Kinondoni ili kusiwe na tatizo la kuingia kituoni
hapo.
Conrad Shio
Afisa Mfawidhi Kanda ya Mashariki
No comments:
Post a Comment