skip to main |
skip to sidebar
KOCHA MKUU WA YANGA HANS VAN DER PLUIJM AMEAGA RASMI NA KUONDOKA KWENDA KUJIUNGA NA TIMU YA AL SHOALAH FC YA SAUDI ARABIA
Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm.
Hans Van Der Pluijm kocha mkuu wa timu ya Young Africans leo amewaaga
rasmi wachezaji wake, viongozi, wapenzi na wanachama baada ya
kumalizaa wake wa miezi sita na sasa anakwenda kujiunga na timu Al
Shoalah FC iliyopo Ligi Kuu nchini Saudi Arabia.
Kocha huyo mdachi ambaye ameiongoza Young Africans kwa kipindi cha
miezi mitano amesema anashukuru kwa sapoti aliyokua akiipata kutoka kwa
wachezaji, viongozi, wapenzi na wanachama wa timu hii kwa kipindi chote
alipokuwa nchini Tanzania.
"Najua wengi itawashangaza kuona naondoka lakini ukweli ni kwamba
niikua na hiyo deal hata kabla ya kuja Yanga, nilikua na makubaliano na
timu ya Al Shoalah FCmakubaliano ambayo yanaanza mwezi ujao hivyo
nilikubaliana na viongozi wa Yanga kuja kufanya kazi kwa kipindi cha
miezi sita tu, nashukuru tumefanya kazi salama na baada ya mkataba huo
kuisha nipo tayari kurudi kuja kufanya kazi Tanzania" alisema Hans.
Naipenda Yanga SC, nimejaza fomu kuomba uanachama hivyo mimi ni
sehemu ya Yanga na katika usajili ujao nitawasaidia kuleta wachezaji
wazuri ambao wataisaidia timu kwenye msimu ujao kwa Ligi ya Vodacom na
mashindao ya Kimataifa.
Kocha Hans anaondoka leo nakwenda Ghana kisha baadae atakwenda nchini
Saudu Arabia tayari kwa kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao katika
timu yangu hiyo ambayo nitaitumikia kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kuhusu usajili kocha mkuu ameshakabidhi ripoti yake ya kiufundi jana, viongozi wanaifanyia kazi kisha baadae itawekwa wazi.
CHANZO: MTANDAO WA YANGA
No comments:
Post a Comment