Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, May 16, 2014

MADIWANI WA CUF WILAYANI URAMBO WASHIRIKI MAPOKEZI YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA NA UJUMBE WAKE


 Madiwani wa Chama cha CUF,wilayani Urambo wakimpokea kwa bashasha kubwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.Shoto ni Diwani wa CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda na kati ni Diwani wa CUF,Kata ya Usoke,Mh.Kadada Mohamed,ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya elimu,afya na maji katika halmashauri ya Urambo mkoani Tabora.Pichani nyuma ya Kinana ni Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye akifurahia jambo.
Diwani wa CUF,Mh.Kandola Nyanda wa kata ya Nsenda akimpokea kwa bashasha kubwa katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwasili katika wilaya ya Urambo,mapema leo akitokea wilayani Sikonge.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora,Mh Fatma Mwasa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Urambo,Mh.Samwel Sitta mara baada ya kuwasili kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana Wilayani Urambo mapema leo.
 Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta akimkaribisha katika jimbo lake Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na ujumbe wake mapema leo.
 Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana akizungumza jambo na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta,Pichani kati ni Mkuu wa Mkoa,Mh.Fatma Mwasa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.

 
  Katibu Mkuu wa CCM ,Ndugu Kinana pamoja na Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta wakishiriki ujenzi wa jengo la maabara katika shule ya sekondari Uyumbu,katika kata ya Uyumbu wilayani Urambo mkoani Tabora-
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Ujumbe wake wakielekea kwenye ukaguzi wa mradi wa jengo la Zahanati ya Izengatogilwe,Wilayani Urambo.Zahanati hiyo itakuwa ina uwezo wa kuhudumia watu wapatao zaidi ya Elfu  mbili,kutoka kijiji cha Izenga,Tebela,Msumbiji na Isongwa. 
 Ndugu Kinana akitoka kukagua moja ya chumba cha zahanati hiyo ya  Izengatogilwe,Wilayani Urambo,yenye uwezo wa kuhudumia watu wapatao zaidi ya Elfu  mbili,kutoka kijiji cha Izenga,Tebela,Msumbiji na Isongwa. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pichani kati,shoto ni Mbunge wa Urambo Mashariki Mh.Samwel Sitta pamoja na Katibu wa NEC Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye wakipata picha ya pamoja na kikundi cha Sungu Sungu
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa akina mama,mashine kati  ya nne za kukamulia mafuta ya Alizeti,Wilayni Urambo mkoani Tabora
 Ndugu Kinana akipata maaelezo mafupi ya mradi huo wa mashine ya kukamulia Alizeti
 Ndugu Kinana akikagua shamba la mahindi linalomwagiliwa kwa njia ya Matone,linalomilikiwa na kikundi cha Hiyari ya Moyo kilichopo katika kijiji cha Ndolobo,Wilayani Urambo. 
 Ndugu Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa jengo la wodi ya akina Mama Wanaosubiri kujifungua,liitwalo Mayulindila.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na vijana wa chipukizi wa CCM,katika mpaka wa Sikonge na Urambo,katika kijiji cha Izimbili,tarafa ya  Usoke Wilayani Urambo kwa ziara ya siku mbili,ambayo itaambatana na wilaya ya Kaliua mkoani Tabora,ambapo Kinana atakuwa na ziara ya siku 11 mkoni humo,ambapo kilele chake itakuwa siku ya jumapili,ambapo mkutano wa hadhara utafanyika.

No comments:

Post a Comment