Wataalamu
wa afya wameonya kuhusu matumizi holela ya mafuta yanayopakwa mwilini
kama dawa za kuzuia mbu, kwa kuwa zinaweza kuwa na madhara kwa baadhi ya
watumiaji.
Kwa
nyakati tofauti wataalamu hao wa masuala ya afya wamesema dawa hizo
ambazo zimekuwa zikitumika kupaka mwilini kama mafuta na matumizi yake
kuongezeka zaidi wakati huu kutokana na tishio la homa ya Dengue,
zinaweza kuwa na madhara kwa sababu mbalimbali.
Daktari
Kiongozi na Mtaalamu wa Homa ya dengue katika Hospitali ya Mwananyamala,
Mrisho Rupinda alisema jana kwamba watumiaji wanapoona madhara ya aina
yoyote wanatakiwa kuchukua hadhari hasa kwa wenye mzio (alerge).
Alisema
kwa kuwa dawa hizo ni kemikali zinahitaji utaratibu na kwa watoto
inahitaji uangalifu mkubwa ambapo ni vyema kuwavalisha nguo ndefu na
iwapo kuna mbu wengi dawa hizo ni vyema zikapakwa juu ya nguo.
Alisema
kwa kuwa ngozi za watoto bado ni changa na laini si vyema kutumia dawa
hizo moja kwa moja kwani zimetengenezwa kwa kemikali zinazoweza kuwa
siyo salama kwa ngozi za watoto.
Alisema wenye vidonda
wanatakiwa kujihadhari kwa kuhakikisha dawa hizo hazigusi vidonda au
sehemu zenye michubuko na inapobidi wapake juu ya nguo, kwa wanawake
wavaa nguo fupi ameshauri kuvaa soksi kisha kupaka dawa hiyo juu yake
kwa kuwa si lazima iguse ngozi.
“Madhara yanaweza kutokea kwa
baadhi ya watu hasa wenye alerge (mzio) na wenye matatizo ya ngozi, ni
vyema kuchukua tahadhari. Madhara yanaweza kutokea kwa yeyote na wakati
wowote,” alisema Dk Rupita.
Mtaalamu wa afya ambaye ni Ofisa
wa Taaluma na Udhibiti wa Magonjwa wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk
Grace Saguti ameonya matumizi yasiyo sahihi ya dawa hizo za kuzuia mbu
mwilini na kusema watumiaji wanatakiwa kupaka kwa kufuata taratibu na si
kutumia kiholela.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa
wiki, Dk. Saguti alisema japokuwa suala hili ni la kitaalamu zaidi watu
wanapaswa kuwa makini kuhusu namna wanavyotumia vizuizi hivyo vya mbu
katika miili yao.
“Vizuizi hivyo vinaweza kuwa na reaction
kutokana na mwili wa mtu. Sitalizungumzia kwa undani zaidi kwa kuwa kila
kitu kina madhara yake lakini watu wasikimbilie kutumia dawa hizo bila
kupata ushauri. Ninajua iwapo mtu atakuwa na vidonda si vyema kutumia
dawa hizo bila kufuata maelekezo kwa usahihi,” alisema.
Kwa
mujibu wa Dk. Saguti, suala hilo la matumizi linahitaji pia tahadhari na
kufuata maelekezo ikiwamo kuhakikisha mwili unakuwa safi wakati wa
kupaka dawa hizo ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza kwenye ngozi.
Matumizi
ya dawa hizo yameshika kasi katika maeneo mengi nchini kwa sasa hasa
kutokana na tishio la ugonjwa wa dengue unaoenezwa na mbu aina ya Aedes
Egyptiae ambao mara nyingi huuma wakati wa mchana.
WAZIRI KOMBO AAGANA NA BALOZI WA IRAN
-
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Mahmoud Thabit Kombo ameagana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislam ya Iran Mhe.
Hossein Al...
8 hours ago
No comments:
Post a Comment