Kutokana na mjadala wa bajeti ya
wizara ya mambo ya nje uliokuwa unaendelea , Mbunge wa Nkasi Ndugu Ali Kessy
ameporomosha matusi mazito kwa wazanzibar kuwa ni watu wa hovyo na ambao kila
mara wanalialia tu kuwa wanabaguliwa , wanadai mambo mengi kuliko uwezo wao na
wakati hawachangii hata senti kwenye Muungano na hivyo kama wanaona wanaonewa
waende kwenye nchi yao sio kukaa kwetu..
Alienda mbali zaidi kusema kuwa
Zanzibar Majimbo ya uchaguzi ni madogo kiasi kwamba ukipigania filimbi wananchi
wote wanakusanyika ila bado wanapewa fedha za mfuko wa Jimbo jambo ambalo sio
haki , na pia hata umeme hawalipi na maji pia .
jambo hili lilimfanya mbunge wa CCM
ndugu Chombo , kuomba muongozo na Kumtaka naibu Spika a mwambie Kessy kamwe
asikanyage Zanzibar , hii ilikuwa baada ya kumuita mwendawazimu , na alisema ni
bahati mbaya kwa CCM kuwa na mbunge mwendawazimu kama huyu ......
Ndugai muda muda wote alikuwa
akicheka , sijui nini maana yake .."...
No comments:
Post a Comment