Serikali inatarajia kuweka katika
mtaala wa elimu unaotumika sasa, somo la afya ya uzazi kwa vijana katika shule
za msingi na sekondari nchini kupunguza mimba za utotoni na maambukizi ya
Ukimwi.Hayo yalisemwa jana, Dar esSalaam na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi,Jenista Mhagama katika ufunguzi wa mkutano wa siku tatu kuhusu
afya ya uzazi kwa vijana
uliozishirikisha nchi 16.Mhagama alisema
serikali imeweka mikakati ya
kuanzisha elimu hiyo ya afyaya uzazi na
jinsia kwa vijanakatika shule za
msingi kutokana na ukubwa wa tatizo
la mimba za utotoni namaambukizi ya
Ukimwi."Serikali inawahakikishia
wanasayansi kuwa elimu hiyo itawapa
matokeo chanya kwamba hakutakuwa
na maambukizi wala mimba za utotoni
kwa vijana hao,'' alisema Mhagama
katika hotuba yake ilisomwa kwa
niaba yake na Mkurugenzi Msaidizi wa
masuala mtambuka katika wizara hiyo,
Letisia Sayi.Mhagama alisema
elimu ya afya ya uzazi kwa vijana
itasaidia kubadili tabia, kujikinga
kwa kutumia kondomu na wanaoishi na
maambukizi kulinda afya zao.Naye,
Mtaalamu wa kitaifa wa masuala ya
Ukimwi na elimu ya afya wa Shirika
la Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO), Martin Herman alisema takwimu.
za wizara hiyo zinaonesha wanafunzi
6000 kila mwaka wanaacha shule kwa
sababu ya mimba za utotoni.Herman
alisema mpango huo wa kutoa elimu ya
afya utaanza Julai mwaka huu baada
ya mapitio ya mtaala huo na
inatarajiwa ifikapo mwaka 2015
wanafunzi watajua afya ya uzazi na
kupata walimu waliobobea katika
masomo hayo.Nchi zilizoshiriki mkutano
huo ni pamoja na Afrika Kusini,
Kenya, Sweden, Uganda, Malawi,
Zimbabwe, Zambia, Burundi, Namibia,
Rwanda, Botswana,
Lesotho,Swaziland, Angola, Ethiopia
na wenyeji Tanzania
No comments:
Post a Comment