MTOTO Nasra Rashid (4) aliyefichwa katika boksi kwa miaka
minne mkoani Morogoro, sasa anaopumulia mashine
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
Nasra, alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili,
alipohamishiwa Mei 26 mwaka huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi akitokea katika
Hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es
Salaam, Daktari bingwa wa Magonjwa ya Watoto, David Kombo, aliyekuwa zamu
alisema Nasra, aliwekewa mashine maalum ili kusaidia kupata hewa ya Oksijeni
baada ya kuanza kupumua kwa shida.
Alibainisha kuwa hali ya mtoto huyo ilikuwa ikiendelea
vizuri lakini juzi usiku ilibadilika na hivyo kuwekewa mashine ya kupumulia.
Dk. Kombo alisema kutokana na hali hiyo, madaktari wa zamu
juzi waliamua kumfanyia vipimo na kubaini anasumbuliwa na Ugonjwa wa Nemonia.
Dk. Kombo, alisema mtoto huyo akipata nafuu ya ugonjwa wa
Nemonia, ataendelea na vipimo vikubwa vya mwili mzima ikiwamo moyo na figo.
Alisema licha ya ya kumpatia dawa za Nemonia, wanaendelea
kumpatia chakula na dawa baada ya vipimo vya awali kubaini ana Utapiamlo.
Ofisa Muuguzi wa zamu, Iluminata Sokani, alisema licha ya
kupumulia mashine hali ya mtoto huyo inaendelea kuimarika kila wanapomfanyia
vipimo kujua maendeleo yake.
Naye mama mlezi wa Nasra, Josephine Joel alisema kabla ya
mtoto hajawekewa mashine ya kumsaidia kupumua, alimuambia anaumia kifuani na
kiunoni
Mtoto Nasra alifichuliwa na Mei 2, mwaka huu na majirani
ambao walimweleza Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha Ndege Dia Zongo kuwa
alikuwa amefichwa katika boksi na Mwanamke aliyetambuliwa kwa jina la Mariamu
Said mkazi wa Kata hiyo mkoani Morogoro.
Majirani hao walimweleza Zongo kuwa Nasra alifichwa ndani ya
boksi tangu akiwa na umri wa miezi tisa 2009 na kwamba hafanyiwi usafi wala
kumtoa nje.
No comments:
Post a Comment