MAKOSA mawili ya Sergio Ramos na Xabi Alonso yameyeyusha matumaini ya Real Madrid kushinda makombe matatu msimu huu.
Real Madrid walikuwa na uwezo kwa kubeba La Liga mbele ya wapinzani wao FC Barcelona na Atletico Madrid, lakini wameshindwa kufanya hivyo baada ya kupigwa mabao 2-0 na Celta Vigo usiku huu.
Kikosi cha Celta Vigo: Alvarez, Jonny, Cabral, Fontas, Aurtenetxe, A Fernandez (A Lopez 56), Krohn-Dehli, Rafinha (Madinda 71), Orellana, Charles (Bermejo 67), Nolito.
Kikos cha Real Madrid: Lopez, Arbeloa (Coentrao 56), Nacho, Ramos, Marcelo, Alonso, Casemiro (Willian Jose 69), Khedira (Illaramendi 56), Modric, Isco, Morata.
Muuaji: Mshambuliaji wa Celta Vigo , Charles alifunga mabao mawili katika ushindi wao wa 2-0 dhidi ya Real Madrid jumapili
Viungo wa Real Madrid, Luka Modric (kushoto) na Xabi Alonso (kulia) hawakutosha kuikoa klabu hiyo na kipigo
Mpepetano ulikuwa mkali, lakini mwisho wa dakika 90, Celta Vigo wameibuka vidume
No comments:
Post a Comment